May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Cristiano Ronaldo arejea Man U

Spread the love

 

BAADA ya kuondoka ndani ya Manchester United ya Uingereza miaka 12 iliyopita, Cristiano Ronaldo (36) ametangazwa kurejea tena ndani ya timu akitokea Juventus ya Italia. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). 

Ronaldo maarufu kama CR7 raia wa Ureno, ametangazwa kurejea viunga vya Old Trafford, alipoondoka mwaka 2009 kwenda kujiunga na vigogo wa Hispania timu ya Real Madrid.

Ronaldo ambaye ameshinda mataji zaidi ya 30, alijiunga na Real Madrid akitokea Manchester United kwa pauni milioni 80 mwaka 2009 na kufunga jumla ya mabao 451 inaelezwa.

Mitandao mbalimbali ya Man U, jioni ya leo Ijumaa tarehe 27 Agosti 2021, imemtambulisha mchezaji bora mara tano wa dunia ‘Ballon d’Or’ mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 na 2017 na kuandika maneno “karibu nyumbani.”

CR7 alikuwa akihusishwa na kutua Man City au PSG ya Ufaransa lakini amekijuta akirejea sehemu alipopata mafanikio makubwa.

Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri alinukuliwa akieleza Ronaldo akimweleza hana mpango tena wa kuwachezea mabingwa hao wa Italia.

Ronaldo alisajiliwa na Manchester United kwa dau la la £12.2m mwaka 2003 akitokea Sporting Lisbon ya Ureno na kufanikiwa kufunga magoli 118 katika mechi 292 akiichezea.

Alihudumu Real Madrid toka mwaka 2009 hadi Julai 2018 alipotangazwa kutimkia Italia na kujiunga na Juventus ambayo hadi anaondoka, ameiwezesha timu hiyo kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo la ligi kuu.

error: Content is protected !!