
Cristiano Ronaldo akipima vipimo vya afya katika klabu ya Juventus
Spread the love
Cristiano Ronaldo akipima vipimo vya afya katika klabu ya Juventus
Picha zilizotolewa na Juve zimemuonyesha nyota huyo akifanya vipimo kabla ya kutambulishwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Allianz.
Juventus watalazimika kulipa pauni 50 milioni kwanza na kumalizia 50 zilizobaki mwisho wa mwaka kwa Real Madrid.
Mamia ya mashabiki wa Juventus wamejitokea kumpokea Ronaldo aliyewasili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya asubuhi.
Mreno huyo aliwasili mjini Turin jana Jumapili akiwa na ndege yake binafsi na leo Jumatatu asubuhi alifika J Medical Centre karibu na Uwanja wa Allianz kwa ajili ya vipimo hivyo.
Ronaldo alisaini jezi kwa mashabiki waliokuwa wakimsubiri na huku wakiimba jina lake. Endapo atafuzu kwa vipimo Ronaldo (33) atambulishwa rasmi kuwa mchezaji Juventus jioni ya leo.
Katika muda wa mchana Ronaldo atakutana na kocha Juventus, Massimiliano Allegri na wachezaji wenzake wapya kukamilisha uhamisho wake kutoka Real Madrid.
Mashabiki wa Juventus walijitokeza nje ya hospitali tangu asubuhi kwa ajili ya kumuona shujaa wao mpya wakiwa na bango yao pamoja na jezi ‘Ronaldo 7’.
More Stories
Namungo yafuzu makundi, yakubali kipigo bao 3-1
Kim Poulsen kutangaza kikosi cha Stars kesho
Waziri Bashungwa aitaka CCM kuwekeza kwenye michezo