July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CRDB kulipa mishahara wafanyakazi

kurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB nchini, Dk. Charles Kimei

Spread the love

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB nchini, Dk. Charles Kimei, amesema watatumia fungu lao la fedha za dharura, kulipa mishahara ya wafanyakazi serikalini endapo itatokea dharura itakayosababisha serikali kushindwa kulipa mishahara kwa wakati. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na kuwalipa mishahara kwa wakati watumishi wa serikali CRDB imeweka utaratibu wa kuwakopesha madiwani tofauti na hapo awali ambapo madiwani walikuwa hawakopesheki.

Kimei aliyasema hauyo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia,aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano maalumu la “Ulipo Tupo”iliyofanyika Kanda ya kati kwa ajili ya kushukuru halmashauri na kudumisha uhusiano.

Hatua hiyo ilielezwa na Dk. Kimei kuwa ilitokana na benki hiyo kupata zabuni ya kufanya kazi na serikali kuu, serikali za mitaa, idara na taasisi mbalimbali za serikali ambayo itadumu kwa miaka mitatu na kwamba idadi kubwa za halmashauri zimekubali kutumia huduma za benki hiyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, Waziri Ghasia amesema asilimia (80%) ya halmashauri zote nchini, zilichagua kuhudumiwa na CRDB na kwamba ikiwa ahadi ya benki hiyo kulipa.

Mishahara endapo serikali itachelewa kutekeleza jukumu hilo kwa wakati, hata zilizosalia zitahamia kwenye benki hiyo.

“Mishahara kulipwa kwa wakati ni moja ya motisha kwa wafanayakazi, lakini kuna wakati mambo yanakwenda ndivyo sivyo mishahara inalipwa nje ya wakati unaotakiwa, kwahiyo CRDB ikiwa na utaratibu wa kusaidia katika suala hili nina hakika waliohamia hawatatoka kamwe, ambao hawajahamia nao watahamia,” alieleza Ghasia.

Awali Dk. Kimei alieleza kwamba kutokana na sababu mbalimbali, kuna wakati serikali huchelewa kulipa mishahara ya wafanyakazi na kwamba hilo likitokea kwa taasisi na idara ambazo zinatumia huduma za benki hiyo, CRDB itatumia fungu lake la dharula kulipa mishahara kwa wakati na kwamba mambo yakikaa sawa serikalini, fedha hizo zitarejeshwa.

Wakati huo huo CRDB imejenga matundu 10 katika shule ya msingi ya Dodoma Makulu yenye thamani y ash.milioni 15.

Kimei alisema hatu hiyo ya ujenzi wa vyoo ni utekerezaji wa miradi mabalimbali ya kijamii kama vile afya,elimu na usafi.

error: Content is protected !!