May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

COVID-19: Waziri Mkuu apigwa faini

Erna Solberg, Waziri Mkuu wa Norway

Spread the love

 

POLISI nchini Norway, limemwadhibu Erna Solberg, waziri mkuu wa nchi hiyo, kulipa faini kwa kuzidisha idadi ya watu pia kupuuza maagizo ya kukaa mbali kati ya mtu na mtu ili kujilinda na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini humo inaeleza, Solberg alifanya sherehe ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa, hivyo alialika wanafamilia 13 nyumbani kwake kuungana naye kwenye sherehe hiyo.

Solberg ametakiwa kulipa faini ya fedha za Norway 20,000 (sawa naTsh.5.2 milioni) kutokana na kupuuza utaratibu huo. Tayari waziri mkuu huyo ameomba radhi kwa kosa hilo.

Serikali ya nchi hiyo iliweka marufuku ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 10. Sherehe ya Solberg ilihusisha watu 13 kinyume na maagizo ya polisi nchini humo.

“Ingawa sheria imewekwa kwa ajili yetu wote, lakini wengine wanatakiwa wawe mbele ya sheria kwa maana ya kutangulia kutekeleza ili kuwa mfano kwa wengine.”

“Ni sahihi kabisa kumpiga faini ili kufanya sheria kuwa na nguvu mbele ya jamii, katika suala la kukaa mbalimbali kama ilivyoelekezwa,” imeeleza taarifa ya polisi.

Polisi wameeleza, Solberg na mumewe Sindre Finnes pamoja na wanafamialia, walikuwa pamoja wakisheherekea lakini ‘mumewe na wengine hatujawapiga faini.”

Polisi wamesema, mume wa Solberg, wanafamilia na wamiliki wa hoteli wote wamevunja sheria ya mkusanyiko, lakini wamempiga faini yeye kwa sababu alitakiwa awe mfano, awaongoze wengine kwa kuwa yeye ni kiongozi wa juu serikalini.

error: Content is protected !!