July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

COVID-19: Serikali yaja na mambo manane

Spread the love

 

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza mambo manane yanayoweza kumsaidia Mtanzania kujilinda na magonjwa ya kuambukizwa ikiwemo virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa leo tarehe 21 Februari 2021, na Gerard Chami, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, imeshauri Watanzania kuzingatia mambo hayo katika kukabiliana na janga la maambukizi yanayotesa dunia kwa sasa.

Mambo hayo ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi tiririka, kutumia vipukusi (sanitizer) mara kwa mara kama hakuna maji tiririka, kufanya mazoezi mara kwa mara na kuwalinda walio kwenye hatari (wazee, watu wanene, wenye magonjwa ya muda mrefu).

Pia kupata lishe bora ikiwemo matunda na mboga mboga, matumizi ya tiba asili zilizosajiliwa na Baraza la Tiba Asili, kuvaa barakoa lakini pia kuwahi kituo cha afya mara unapohisi dalili za maradhi ili kusaidiwa.     

“Ni vyema kila mmoja akawa na utaratibu wa kupima afya yake mara kwa na kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni za mtindo bora wa maisha ili kuondoa vihatarishi vya kiafya vinavyodhoofisha kinga ya mwili.

“Kila mmoja wetu ajione ana jukumu la kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza na yale ya kuambukiza,”  amesema Chami.

error: Content is protected !!