July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Covid-19: Mbowe ataka vigogo wizara ya afya Tanzania wajiuzulu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima

Spread the love

 

MWENYEKITI wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania- Chadema, Freeman Mbowe, amemtaka Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima na wasaidizi wake, wajiuzulu kwa kushindwa kuongoza vyema mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona. Anaripoti Mwandisi Wetu, Mwanza … (endelea).

Wengine ni; Naibu waziri wake, Dk. Godwin Mollel pamoja na makatibu wakuu na naibu wao wa wizara hiyo.

Mbowe ametoa wito huo leo Jumatatu, tarehe 19 Julai 2021, akizungumza na wanahabari jijini Mwanza.

“Sayansi ni sayansi na Mungu wetu ni Mungu wetu, tusimuingize Mungu kwenye vsihawishi ambavyo havina kichwa wala miguu, Serikali ileile na waziri walewale wa afya waliohimzia mitishamba, leo wanatuambia kuna corona,” amesema Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa Chadema amedai kuwa, waziri huyo na wasaidizi wake walishindwa kuliongoza vyema Taifa katika kukabiliana na janga hilo, linalosababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19).

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Mbowe amedai kuwa, katika wimbi la kwanza la mlipuko wa Covid-19, Dk. Gwajima na wasaidizi wake, walishindwa kufuata njia za kisayansi zinazoshauriwa na wataalamu wa afya, ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO), ikiwemo kuhimiza kuvaa barakoa na kutoa takwimu za mwenendo wa ugonjwa huo.

Amesema, katika wimbi la kwanza wizara hiyo ilishindwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu uwepo wa Covid-19, hali iliyopelekea sasa hivi kupuuza kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

“Katika nchi yenye uwajibikaji, waziri wa afya na naibu wake na makatibu. Hawa watu wangeshaachia ofisi ya umma muda mrefu sana, walidanganya watu. Hata leo Watanzania wengi ukiwaambia kuna tatizo la Covid-19 wanaona utani,” amesema Mbowe na kuongeza:

Mbowe ameongeza “mawaziri wale wako ofisini wanatuzungumzia kujikinga, tunauwa na kuzika watu, watu wanaona mambo ya kawaida.”

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Dk. Godwin Mollel

Mara ya mwisho, Waziri Gwajima kutoa takwimu za wagonjwa wa corona ni tarehe 10 Julai 2021, akisema kuna wagonjwa 408 nchi nzima wa corona.

Tayari Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekuwa akisisitiza wananchi kuchukua tahadhari ya maambukizi hayo, ikiwemo kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kunawa mikono na maji tiririka.

error: Content is protected !!