May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

COVID-19: Magogo ya kuchomea watu India yaadimika

Spread the love

 

IDADI kubwa ya vifo vinavyotokana na virusi vya corona (COVID – 19), nchini India, imesababisha uhaba wa magogo ya kuchomea watu. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Taarifa zinaeleza, India inataabika na uhaba wa magogo kwa kuwa, idadi ya watu wanaokufa na kuhitaji huduma hiyo kulingana na Imani yao, imekuwa kubwa nchini humo.

India kwa sasa ndio nchi namba moja kuwahi kutokea katika kurekodi idadi kubwa ya maambukizi ndani ya siku moja na ongezeko la kasi la vifo.

Tofauti na nchi zilizowahi kushika nafasi za juu katika kurekodi maambukizi mapya – Marekani, Brazil na Mexico – sasa India inarekodi zaidi ya watu 300,000 kwa siku huku idadi ya vifo ikiongezeka.

Katika Mji Mkuu wa nchi hiyo – Delhi, eneo la maegesho ya magari limegeuzwa na kuwa sehemu ya kuchomea watu wanaofariki dunia kulingana na Imani yao.

Idadi kubwa wagonja nchini humo wanataabika na kupata huduma ya mtungi wa gesi ya oksijeni ili kuwasaidia kupumua. Kwa sasa India tatizo si kuwa na pesa ya kupata huduma hiyo, bali upatikanaji wa huduma hiyo. kili

Kwa siku saba mfululizo, India imerekodi zaidi ya maambukizi 300,000 kwa siku, hali inayotishia usalama wa taifa hilo lililo na watu bilioni 1.4.

Jumapili wiki iliyopita, Waziri wa Afya wa India, Dk. Harsh Vardhan alieleza taifa hilo kurekodi maambukizi mapya 360,960 katika saa 24 na kuweka rekodi ya kuwa na maambukizi milioni 18 katika taifa hilo. Siku hiyo waliofariki dunia ni 3,293.

error: Content is protected !!