Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko COVID-19: India inazama, Tanzania yasisitiza umakini
Habari Mchanganyiko

COVID-19: India inazama, Tanzania yasisitiza umakini

Spread the love

 

WAKATI Taifa la India likizama katika maambukizi ya virusi ya corona (COVID-19), na kushika namba moja duniani, Serikali ya Tanzania imesisitiza wananchi kuchukua tahadhari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Tahadhari hiyo imetolewa na Wizara ya Afya kupitia Prof. Abel Makubi, Mganga Mkuu wa Serikali huku akisisitiza matumizi ya vipukusi, kuvaa barakoa pamoja na kunawa mikono.

Kwenye taarifa yake, Prof. Makubi amesema virusi vya corona vitaendelea kuwepo, hivyo wananchi wanapaswa kujivunza kuishi maisha kwa kuzingatia kuwepo kwa tishio hilo.

Na kwamba, wananchi hao wanapaswa kuondoa hofu huku wakiendelea kuchukua hatua muhimu za kujikinga na virusi hivyo.

Ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua hiyo, Prof. Makubi amesisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi, kupata lishe bora ili kuimarisha kinga mwili sambamba na kutumia tiba asili zilizodhibitishwa na Baraza la Tiba asilimia.

Prof, Abel Makubi Mganga mkuu wa Serikali

“Tambua afya yako, jilinde tukulinde. Wito huu unawahusu makundi maalum wakiwemo wenye uzito mkubwa, wazee, wenye magonjwa mbalimbali sugu ya muda mrefu kama pumu.

“Pia unawahusu wenye shinikizo la juu la damu, kisukari magonjwa ya ini, figo, moyo nasi tutaendelea kuimarisha huduma za wazee na kliniki za magonjwa sugu,” amesema.

Prof. Makubi ametokana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa huo pia kuunda kamati kwa ajili ya kuja na mpango mkakati wa kupambana na gonjwa linalotikisa dunia kwa sasa.

India kwa sasa ndio taifa lililoathirika Zaidi na maambukizi ya corona, kwani kwa siku moja maambukizi yanavuka watu 300,000.

Kabla ya India kushika nafasi ya juu katika maambukizi, awali nafasi hiyo iliwahi kushikwa na Marekani, Brazil na Mexico.

Mpaka kufika leo tarehe 30 Aprili 2021, maambukizi ya virusi vya corona duniani yamefika 151,159,899, vifo vikiwa 3,179,925 na waliopona 128,571,189.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!