Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa COVID-19: Idadi ya vifo yatisha India
Kimataifa

COVID-19: Idadi ya vifo yatisha India

Spread the love

 

IDADI kubwa ya watu wanaoripotiwa kuambukizwa virusi vya corona (COVID-19) na kufariki dunia kwa siku nchini India, inatisha. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Katika siku za karibuni, nchi hiyo imekuwa ikiripoti maambukizi ya watu 150,000 kwa siku moja, tofauti na miezi miwili iliyopta.
Lakini leo tarehe 26 Aprili 2021, maambukizi mapya 350,179 ya corona yameripotiwa, hivyo kufanya jumla ya idadi ya walioambukiza kwenye taifa hilo kuwa milioni 17 na kushika namba mbili kwa maambukizi duniani ikitanguliwa na Marekani.

Katika saa 24 zilizopita, India imepoteza watu 2,812 waliofariki kutokana na corona. Hata hivyo, taarifa zinaeleza namba hiyo yaweza kuwa kubwa zaidi.

Kusanyo la taarifa za awali zimeeleza, Januari na Februari nchi hiyo ilikuwa ikiripoti maambukizi 20,000 kwa siku, lakini sasa idadi hiyo imeongezeka kwa kiwango kikubwa na kwa kasi zaidi.

Kuongezeka kwa kasi hiyo, kumesababisha hospitali nchini humo kufurika huku huduma ya vitanda, mitungi ya gesi pamoja na dawa kuwa tabu kupatikana.

Taarifa zaidi zinaeleza, wagonjwa wengine waliofanikiwa kupata mitungi ya gesi, wamekuwa wakiitumia majumbani mwao huku wale waliokosa huduma hiyo, wanafariki dunia.

Taifa hilo lenye watu Bil 1.4, limekuwa na rekodi mpya na mbaya zaidi katika siku za karibuni kutokana na kiwango kikubwa cha watu wanaoambukizwa virusi hivyo.

Saket Tiku, Rais wa Viwanda vya Gesi nchini humo amesema, tatizo kubwa linaloikabili India kwa sasa, ni kusafirisha gesi ya Oxygen kwa haraka eneo inapohitajika.

Hadi leo mchana Jumatatu, maambukizo duniani yamefikia milioni 147.84, waliofariki wakiwa milioni 3.12 na waliopona ugonjwa huo milioni 125.42.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!