Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa COVID-19: DRC yasitisha chanjo ya AstraZeneca
Kimataifa

COVID-19: DRC yasitisha chanjo ya AstraZeneca

Waziri wa Afya WA DRC, Eteni Longondo
Spread the love

 

SERIKALI ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imeahirisha kampeni ya kutoa chanjo ya AstraZeneca, ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya Kimataifa.

DRC imepokea dozi zaidi ya milioni 1.7 ya chanjo hiyo, iliyokuwa ianze kutolewa kesho Jumatatu tarehe 15 Machi 2021.

Waziri wa Afya, Eteni Longondo amesema wameamua kuahirisha tarehe ya uzinduzi wa chanjo hiyo kama hatua ya tahadhari, baada ya nchi nyingine kadhaa kufanya uamuzi kama huo.

Nchi ambazo zimesitisha utoaji wa chanjo hiyo kwa madai kwamba inasababisha damu kuganda ni; Norway, Thailand, Bulgaria, Denmark na Iceland ili kufanya uchunguzi zaidi.

Waziri Longondo huyo amesema, tarehe mpya ya uzinduzi wa chanjo hiyo itatangazwa baada ya uchunguzi wa kiserikali na wa Kimataifa.

Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO), limesema chanjo hiyo ni salama, na hakuna ushahidi kuwa inasababisha madhara hayo.

AstraZeneca imesema, usalama wa dawa umefanyiwa utafiti mkubwa katika majaribio ya tiba, ikiwa ni pamoja na katika maabara za Ureno, Australia, Mexico na Ufilipin, wamesema wanaendelea na mpango wa utoaji wa chanjo.

Mataifa mengine ambayo yanataka kusitisha mi pamoja na Uingereza, Ujerumani, Mexico na Australia

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mpinzani mkuu wa Rais Kagame aachiwa huru

Spread the love  PAUL Rusesabagina, aliyewahi kuripotiwa kama ‘shujaa’ katika filamu ya...

Kimataifa

Rais Tshisekedi amteua kiongozi wa wanamgambo kuwa Waziri wa Ulinzi

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi,...

Kimataifa

Raila Odinga: Tutafanya maandamano makubwa mara mbili kwa wiki

Spread the love KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Raila Amollo Odinga ametangaza...

Kimataifa

Magharibi kuwekeza silaha Indo-Pacific, China yachochea

Spread the love KUVUNJIKA ushirhikiano wa China na Magharibi uliodumu kwa takribani...

error: Content is protected !!