ASKOFU Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametoa tahadhari kwa serikali juu ya chanjo ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Akichangiwa wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka 2021/22, Askofu Gwajima amesema, Taifa linatakiwa kuchukua tahadhari kabla ya kuruhusu chanjo ya corona kwa wananchi.
Amesema, hapingani na chanjo ya corona, lakini amesisitiza umakini katika aina ya chanja iwapo Tanzania itataka kuridhia.
Kwamba, kumekuwa na ‘chanjo mwendo kasi,’ ambapo inapohojiwa sababu ya haraka hiyo, “najibiwa kwa sababu teknolojia imekuwa.”
Askofu Gwajima amesema, chanzo za sasa zimechukua muda mchache kulinganisha na chanjo nyingine miaka ya nyuma, kwamba zilichukua mpaka miaka 10 kabla ya kuingizwa sokoni.
Amesema, chanzo zinazotumika sasa, zimeruhusiwa na mamlaka ya dharura ambao wanadai, madhara yanayotokana katika chanjo ni kutokana na mtumiaji mwenyewe.
Leave a comment