June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

COSTECH haikutengewa fedha- Malima

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima

Spread the love

SERIKALI imesema katika bajeti ya mwaka huu, kuna fedha iliyotengwa kwenda  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kwa ajili ya kuwawezesha watafiti nchini kufanya kazi yao kwa ukamilifu. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo, imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Haroub Mohamed Shamis (CUF) ambaye alitaka kujua serikali inasema nini katika kuwawezesha watafiti makini wa Tanzania kwa kuwapatia vitendea kazi na fedha ili waweze kufanya tafiti sahihi.

Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Lushoto, Dk.Henry Shekifu (CCM), alitaka kujua Tanzania ina mpango gani wa kuanzisha kilimo cha Uhandisi Jeni (GMO), kinachoonyesha kuongeza uzalishaji mara dufu katika mazao ya pamba na mengineyo.

Pia alitaka kujua kama wataalam wa Tanzania wamejifunza utaalamu huo na wanatoa ushauri gani kwa aina hiyo ya kilimo.

Akijibu kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Pindi Chana amesema, wataalam wa Tanzania wamejifunza utaalamu huo na wanao uwezo wa kuitumia teknolojia hiyo ambapo katika utafiti wa maabara kwa kutumia uhandisi jeni wameanza kugundua jeno katika muhogo ambazo zina ukinzani wa magonjwa ya batobato na michirizi kahawia ya muhogo.

Pindi amesema, kwa sasa watafiti hao wanaendelea na utafiti huo katika ngazi ya mashamba maalumu ili kuwawezesha kugundua aina za muhogo ambazo zina ukinzani dhidi ya magonjwa hayo.

“Kwa kuzingatia manufaa ya uhandisi jeni katika kilimo wataalam wamekuwa wakishauri matumizi ya teknolojia hiyo kama matokeo ya utafiti yataonyesha kuwa matumizi ya mazao ya GMO ni salama na hayana madhara yoyote kwa binadamu, wanyama na mazingira,” amesema.

Aidha, amefafanua kuwa, serikali itaendelea kuwaelimisha na kukuza uelewa kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kuhusu manufaa ya teknolojia ya uhandisi jeni katika maendeleo ya kilimo.

error: Content is protected !!