January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Cosota yawataka wachoraji kupanua soko

Spread the love

CHAMA cha Hakimiliki Tanzania (Cosota), kimetoa rai kwa wasaniii wa sanaa za uchoraji kupanua soko la sanaa kwa kutafuta mikataba ya kimataifa. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, baada ya mkutano wa kusaini mkataba kati ya kikundi cha sanaa ya uchoraji cha Tingatinga Arts na kampuni ya Bricoleur kutoka Japan.

Afisa mtendaji wa chama hiko, Doreen Sinare amesema ni muhimu kwa wasanii kuwa na ubunifu na kutafuta soko la nje kwa sababu wateja wengi wa sanaa za uchoraji wanatoka nje ya nchi.

Sinare amesema kuwa wasanii wa sanaa ya uchoraji wanapaswa kutazama mfano wa utendaji kazi wa kikundi hiko katika soko la kimataifa ndani ya mkataba huo wa miaka mitano uliosainiwa na Mwenyekiti wa kikundi cha Tingatinga, Zachi Chimwanda.

“Huu ni mkataba wa kuigwa na wasanii wanapaswa kuangalia na kupima mwenendo wake ili nao kutafuta soko zaidi na kuitangaza Tanzania,” anasema Sinare.

Naye Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amesema kupitia mkataba huo wasanii wa sanaa za uchoraji wa Tingatinga watanufaika kujitangaza na kujipatia kipato cha mmoja mmoja kulingana na ufanyaji kazi wao.

“Wasanii wanatakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kuliteka soko la kimataifa hivyo sisi kama baraza la sanaa la Taifa tunaunga mkono jitihada hizi kwani kazi nzuri za watanzania imeanza kuonekana,” amesema Mngereza.

error: Content is protected !!