July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

COSOTA kukusanya, kugawa mirabaha ya Bil. 1.3/- mwaka 2022/23

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa

Spread the love

 

TAASISI ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) inatarajia kukusanya mirabaha yenye thamani ya Sh.1.3 bilioni na kuigawa kwa wabunifu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu tarehe 6 Juni, 2022 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumiz kwa mwaka 2022/23.

Serikali kupitia COSOTA ilianza rasmi kutoa mirabaha kwa kazi za ubunifu mwaka huu fedha ambapo jumla ya Sh. 312 milioni ziligawanywa kwa Wasanii na Wanufaika 1,123 wa ndani na nje ya nchi.

Katika mgao huo kazi za muziki 5,924 zilitumika hapa nchini na nje ya nchi.

Katika utoaji huo wa mirahaba, kwaya ya Mt. Cecilia iliibuka namba moja kwa kupokea Sh. 8.7 milioni, huku ikifuatiwa na msanii Ali Kiba Sh. 7 milioni , na namba tatu ni mwana mama Rose Muhando aliyejizolea Sh. 5.7 milioni.

Mbali na ugawaji wa mirabaha mwaka ujao wa fedha Serikali imejipanga kutoa leseni 1,490; kufanya usajili wa kazi zisizopungua 2,500 na wabunifu 500.

error: Content is protected !!