September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Corona yawaibua shirika la usawa wa kijinsia

Baadhi ya washiriki wa semina ya Usawa wa Kijinsia

Spread the love

SHIRIKA la Usawa wa Kijinsia leo limeendesha semina ya siku mbili kwa waathirika wote wa maswala ya jinsia katika sehemu zao za kazi na makazi, haswa kwenye kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Semina hiyo ya siku mbili kuanzia 23 mpaka 24 Julai, 2020, ikiwa na washiriki zaidi ya 50 ambayo inafanyika jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shirika hilo, Jamaica Adam amesema lengo la semina hiyo ni kuangalia mambo ya ukatili wa kijinsia yaliyojitokeza wakati wa ugonjwa wa Covid-19 kwa wafanyakazi wa ndani, Bar na wafanyabiashara ndogondogo (mama ntilie). 

“Kipindi hiki cha Covid-19 kuna ukatili umejitokeza kwenye maeneo mbalimbali kama mabaa na wafanyakazi wa ndani kwa kutolipwa stahiki zao kwa kigezo cha uwepo janga hilo la Covid-19,” alisema mratibu huyo.

Aidha aliendelea kwa kusema kuwa semina hiyo haitaishia kwa makundi hayo bali itashuka mpaka kwenye ngazi ya mtaa ambapo wanapatikana maafisa wa Ustawi wa Jamii ili kuwapa elimu wakaisambaze katika maeneo hao.

Baadhi ya washiriki wa semina ya Usawa wa Kijinsia

“Ukiacha makundi haya lakini pia tumelenga kamati za serikali za mitaa ambazo zinahusisha M/kiti pamoja na dawati la jinsia ili tuwape elimu wakaweze kusambaza katika jamii yao ili waweze kupata uwelewa,” aliongezea Jamaica.

Kwa upande wake, Arapha Suleiman ambaye ni mmoja wa washiriki wa semina hiyo amesema kuwa dhumuni la kuudhuria semina hiyo ni kujifunza na kupeleka elimu katika jamii ya namna ya kuzuia maswala ya ukatili wa kijinsia hasa kwa upande wa watoto.

“Mimi nazunguka sehemu nyingi na naona namna watoto kambo wanavyo nyanyasika mitaani kwa walezi kukosa elimu ya kijinsia na namna bora ya kuwalea watoto ili kuweza kuwandaa katika maisha yao ya kesho,” alisema Arapha.

Semina hiyo inayotarajiwa kufungwa kesho jijini Dar es Salaam na kuanza kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.

error: Content is protected !!