June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Corona yaua 29 Tanzania, Dk. Gwajima “tuchukue tahadhari”

Waziri wa Afya nchini Tanzania, Dk. Dorothy Gwajima

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema, mpaka sasa wagonjwa 29 walioambukizwa virusi vya corona (COVID-19), wamefariki dunia. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri wa Afya nchini humo, Dk. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema, “jana peke yake kwenye vituo vyetu wako wagonjwa 176 wa corona. Na hawa ni waliokwenda vituoni, wapo ambao wapo majumbani.”

Amesema, idadi hiyo ya vifo ni hadi tarehe 21 Julai 2021 ambapo hadi sasa kuna wagonjwa zaidi ya 600 wa corona kwenye mikao mbalimbali nchini.

Waziri Gwajima amewaomba wananchi na viongozi mbalimbali kuchukua tahadhari ya virusi hivyo na kuacha mzaha kwamba wimbi la kwanza na la pili lilipita na hili la tatu litapita.

“Nawakumbusha wanaoendelea kufanya mzaha na corona. Wako wanaosema mbona wimbi la kwanza na la pili lilipita na hili la tatu litapita, nawasihi sana tusichukulie kwa wepesi tuchukue tahadhari,” amesema Waziri Gwajima

Waziri huyo amesema kwa hali ilivyo sasa anashanaga jinsi mamlaka zingine zinavyouchukulia ugonjwa huo ikiwemo wanaohusika na usafirishaji magari kuendeleza kujaza, mikusanyiko kama ya burudani na michezo.

Waziri wa afya nchini Tanzania, Dk. Dorothy Gwajima kesho Jumamosi atatoa taarifa kuhusu chanjo ya maammbukizi ya virusi vya corona inapatikana wapi na taratibu zingine.

error: Content is protected !!