Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Corona yatibua dili la Harmonize Ulaya
Michezo

Corona yatibua dili la Harmonize Ulaya

Harmonize
Spread the love

 

MSANII wa Bongofleva, Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize au Kondeboy amewaomba radhi mashabiki wake baada ya kubadili ratiba ya ‘tour’ (ziara) yake kwenye baadhi ya nchi za bara la Ulaya na Amerika Kaskazini kutokana na masharti ya virusi vya Corona. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Harmonize ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema leo tarehe 22 Septemba 2021, akiwa huko jijini Las vegas nchini Marekani.

Aidha, CEO huyo wa lebo ya Konde Music World Wide anaendelea na tour yake kwenye baadhi ya maeneo nchini humo.

Msanii huyo amesema, “watu wangu wa Canada na Sweden naomba radhi kwa kuwa nimeshindwa kukamilisha ratiba ya tarehe tuliyoipanga kwa sababu ya vizuizi vya Uviko 19″

Hata hivyo, msanii huyo amesema atatoa tarehe mpya hivi karibuni kwa wale mashabiki wake ambao tayari walishakata tiketi kwe ajili ya kwenda kuwapa burudani kama ilivyopangwa.

Pia Harmonize ametangaza kuendelea na tour yake kwenye maeneo yaliyobakia ambayo hayana vizuizi vya Uviko 19.

Kwa mujibu wa ratiba yake, tarehe 23 Septemba atakuwa Las Vegas, Oktoba mosi – New York, Tarehe 9 Oktoba – Los Angels, 15 Oktoba- Idaho, 22 Oktoba – Minnesota na 23, Oktoba – Suracus New York.

Hadi sasa ameshakamua katika majimbo ya Ohio, Huston Texas, Pheonix, na Los vegas na mengine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!