Saturday , 20 April 2024
Kimataifa

Corona: WHO yatoa onyo

Spread the love

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limetoa tahadhari kwa dawa za mitishamba zinazotengenezwa ili kukabiliana na virusi vinavyosababisha homa ya mapafu (corona). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

WHO imetoa taarifa hiyo wakati ambao baadhi ya mataifa ya Afrika yakijielekeza nchini Madagascar kuchukua dawa iliyotengenezwa kwa mitishamba.

Shirika hilo limeeleza, kwamba ni vizuri dawa ni muhimu dawa zinazosemekana kuwa na uwezo wa kutibu, kufanyiwa majaribio kwanza.

“…huenda watu wakaona wamepata tiba na kujihisi kuwa salama, ikiwa watakuwa na imani na dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio,” wameeleza.

Miongoni mwa nchi zilizoeleza wazi kutumia dawa iliyopatikana nchini Madagascar ni Tanzania, Jamuhuri ya Congo, Guinea Bissau na Equatorial Guinea.

Mataifa haya, yameeleza wazi kwamba watatuma ndege nchini Madagascar kuchukua dawa hiyo ya mitishamba.

Dawa hiyo inayohusishwa na mmea wa Kichina unaoitwa Artemisia (pakanga), mmea huo ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!