BORIS Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza amekimbizwa hospitali kutokana na makali ya virusi vya corona (COVID-19). Linaripoti Shirika la Habari la BBC.
Boris alikimbizwa hospitali jana Jumapili usiku katika hospitali moja ya mjini London. Amepelekwa ikiwa ni siku 1 baada ya kubainika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo alipokuwa ofisini kwake Downing Street.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya joto mwilini kupanda zaidi, meonekana. Kutokana na joto hilo, daktari wa Boris alishauri apelekwe hospitali.
Kutokana na hatua hiyo, waziri wa maswala ya kigeni nchini humo, Jeremy Hunt anatarajiwa kuongoza mkutano wa virusi vya corona leo.
Ijumaa wiki iliyopita Boris aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter “Bado nina joto mwilini. Hivyo basi kulingana na ushauri wa serikali, ninafaa kuendelea na karantini hadi pale dalili hizo zitakapopotea,’ na kuongeza ”hata hivyo, tunafanya kazi muda wote ili kuvishinda virusi hivi.”
Leave a comment