September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Corona: Saa 24 watu 572 wafariki A. Kusini

Spread the love

SAA 24 zilizopita, watu 572 wameripotiwa kufariki dunia nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti BBC … (endelea).

Baraza la Utafiti wa Tiba nchini humo limeeleza, kwamba upo wasiwasi idadi ya waliofariki ikawa kubwa zaidi ya hiyo kutokana na vifo vingine kutoripotiwa.

“Tuna wasiwasi kuwa, huenda idadi ya waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona ni kubwa zaidi kuliko takwimu zinavyoonesha,” limeeleza baraza hilo.

Tafiti za majuma 10 yaliyopita zinaonesha, kumekuwa na vifo 17,000 zaidi kuliko kawaida na kwamba, kuna vifo 11,000 ambavyo havijaelezwa.

error: Content is protected !!