Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari Corona: Ni hekaheka Maabara ya Taifa
Habari

Corona: Ni hekaheka Maabara ya Taifa

Spread the love

DAKTARI Nyambura Moremi, Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na Jacob Lusekjelo, Meneja Udhibiti wa Ubora wamesimamishwa kazi kufuatia tuhuma zilizotolewa na Rais John Magufuli. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Jana tarehe 3 Mei 2020, wakati akimwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Rais Magufuli alionesha mashaka kuhusu utendaji kazi wa maabara hiyo na kuagiza ufanywe uchunguzi.

Akizungumzia mkanganyiko wa matokeo ya sampuni mbalimbali za zilizohusu maambukizi ya virusi vya corona, Rais Magufuli alisema maabara hiyo imekuwa ikitoa majibu yenye mkanganyiko.

“Waziri nimekuapisha leo, itabidi mkafanye uchunguzi katika laboratory (Maabara) ya kitaifa ya Tanzania iliyokuwa inahusika kupima corona,” alianguza Rais Magufuli na kuongeza:

“Ukishagundua kitu hiki, lazima ujue kuna mchezo wa ajabu unafanika katika vipimo hivi. Kwamba kuna mambo ya ajabu yanafanywa katika nchi hii, eidha wahusika wa laboratory (maabara) ile wamenunuliwa na mabeberu.

“…eidha hawana utaalamu whichi is not true (kitu ambacho si kweli) kwasababu maabara hii imetumika sana kwenye magonjwa mengine…”

Taarifa iliyotolewa na Waziri Ummy leo tarehe 4 Mei 2020, imeeleza kuwasimamisha viongozi hao ili kupisha uchunguzi kuhusu sakata la vipimo hivyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Catherin Sungura, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Idara Kuu-Afya.

Taarifa hiyo imeeleza “kufuatia hotuba ya Rais Magufuli wakati akimwapisha Waziri wa Katiba na Sheria alibainisha changamoto za utendaji wa Maabara ya Taifa ya Jamii, Waziri Ummy amechukua hatua na kumwagiza katibu mkuu afya, kuwasimamisha kazi mara moja Dk. Moremi na Lusekelo, ili kupisha uchunguzi,” inaeleza taarifa ya Sungura.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sungura, Waziri Ummy ameunda kamati ya wataalam  kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa mwenendo wa maabara hiyo, ikiwemo mfumo mzima wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za COVID-19.

Waziri Ummy ameagiza kamati hiyo kuwasilisha taarija juu ya uchunguzi huo ndani ya siku tisa, kuanzia leo hadi tarehe 13 Mei mwaka huu.

“Sambamba na uchunguzi wa kamati hii, shughuli za upimaji wa sampuli katika maabara hii zinaendelea,” inaeleza taarifa ya Sungura.

Wajumbe wa kamati hiyo ni Prof. Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS), Prof. Gabriel Shirima wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela (NMIST), Prof. Steven Mshana kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Bugando (CUHAS).

Wengine ni Prof. Rudovick Kazwala kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), na Dk. Thomas Maranduwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!