April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Corona: Mbunge ‘Bunge lifungwe’

Spread the love

HOFU ya kusambaa kwa virusi vya corona (COVID-19), ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa inazungumzwa waziwazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ikiwa Bunge na Watanzania wakiwa kwenye majonzi ya kumpoteza Richard Ndassa, aliyekuwa Mbunge wa Sumve, Mwanza, ushauri unatolewa wa kulifunga bunge hilo kwa siku 14.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge, Juma Nkamia ambaye ni Mbunge wa Chemba jijini Dodoma, amemshauri Job Nduga, Spika wa Bunge kuona uezekano wa kulifunga Bunge kwa siku 14 ili kila mbunge ajiweke karantini kuangalia kama amepata maambukizi ya corona.

Ushauri huo unatolewa wakati virusi hivyo vikielezwa kuua katiba bunge hilo.

“…hapa Dodoma, moja ya watu tuliokuwa nao karibu sana, labda mimi, Mwambalasa na Ndassa. Hata wakati mwingine vijiwe vya jioni tunakaa pamoja,” amesema Nkamia akiongeza kwamba, kifo cha Ndassa ni pengo kubwa.

Amesema, “…lazima sasa hatua kali zichukuliwe, hapa bungeni tuna mchanganyiko mwingi na hauwezi kumjua nani ambaye ameathirika.

“Hata uongozi wa Bunge uamue kusitisha Bunge walau kwa siku 14, kila mbunge ajikarantini. Lakini tukifanya hivi holela holela, itatugharimu sana.”

error: Content is protected !!