May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Corona: Maambukizi mapya yashtua Uganda

Spread the love

 

JUMLA ya watu 126 nchini Uganda wameripotiwa kufariki dunia ndani ya siku nne zilizopita kutokana na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Idadi hiyo ni kubwa katika kipindi kichache ambapo mpaka sasa, watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo wamefika 752.

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza, idadi kubwa ya watu wanaofikishwa hospitali kuopata huduma hiyo, wanakuwa katika hali mbaya jambo lililosababisha kuongezeka kwa vifo hivyo.

Dk Charles Olaro, Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu Wizara ya Afya Uganda amesema “wimbi la tatu la corona ni baya zaidi na watu wana tabia ya kufika katika vituo vya afya wakiwa katika hali mbaya.”

Inaelezwa, vifo hivyo (126), ni asilimia 16.7 ya jumla ya vifo vilivyoripotiwa  nchini humo tangu ugonjwa huo kuingia Uganda mwaka jana.

Vifo hivyo ni sawa na asilimia 16.7 ya jumla ya vifo vilivyoripotiwa tangu kulipuka kwa ugonjwa huo mwaka 2020.

Taarifa kutoka Uganda zinaeleza, kati ya sampuli 7,196 zilizopimwa virusi vya corona tarehe 21 Juni 2021, watu 859 walikutwa na maambukizi. Idadi hiyo inafanya waliopimwa na kukutwa a corona kufika 74,260.

error: Content is protected !!