April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Corona janga la dharura – WHO

Spread the love

TEDROS Adhanom, Kiongozi Mkuu wa Shirika la Afya duniani (WHO), ametangaza kwamba virusi vya Corona sasa ni janga la dharura duniani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Adhanom amesema “watu takribani 213 wamefariki kutokana na virusi hivyo nchini China.”

Amesema, WHO limedhibitisha, kwamba kumekuwa na visa 98 katika mataifa mengine 18 ingawa hakuna vifo virivyoripotiwa. Visa vingi vya wagonjwa hao vilitokana na watu waliosafiri kutoka mji wa Wuhan, China eneo ambalo mlipuko wa ugonjwa huo ulipoanzia.

“Sababu kubwa ya tangazo hilo si kwa sababu ya kile ambacho kinatokea China kwa sasa, lakini kile ambacho kinatokea katika mataifa mengine,” amesema Adhanom.

Hata hivyo, Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya nchini Tanzania amesema, mtu yeyote atakayepata virusi vya Corona ndani ya Tanzania, atatibiwa katika maeneo yaliyotengwa yaliyopo mkoani Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza na kwamba, mpaka sasa hakuna mkasa wa virusi hivyo nchini.

error: Content is protected !!