Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Corona inavyoendelea kuitesa Afrika, dunia 
Habari Mchanganyiko

Corona inavyoendelea kuitesa Afrika, dunia 

Spread the love

MAAMBUKIZO ya virusi vya corona (COVID-19) duniani, yamefikia milioni 85.5, waliopona milioni 60.4 na waliopoteza maisha milioni 1.8. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hadi leo Jumatatu asubuhi tarehe 04 Januari 2021, Marekani inaongoza kwa maambukizo mengi duniani yaliyofikia milioni 21.1, waliofariki 360,078 na waliopona milioni 12.4.

India inashika nafasi ya pili ikiwa na maambukizo milioni 10.3, waliopona milioni 9.9 na waliofariki wakiwa 149,686.

Brazil ina maambukizo milioni 7.7 ikiwa nafasi ya tatu, waliofariki kutokana na ugonjwa huo wakiwa 196,018 na waliopona milioni 6.8.

Barani Afrika, Afrika Kusini, inaongoza kwa kuwa na maambukizo milioni 1.1, waliopona 903,679 na waliofariki wakiwa 29,577.

Morocco inashika nafasi ya pili Afrika ikiwa na maambukizo 443,146, waliopona 413,393 na vifo vikiwa 7,485.

Nchi za Afrika Mashariki, Kenya inaongoza kwa kuwa na maambukizo 96,802, waliopona 79,073 na vifo vikiwa 1685.

Kutokana na maambukizo hayo, baadhi ya mataifa, yamekuwa yakiweka mazuio ya kutosafiri au kutoka nje kwa kipindi Fulani ili kuzuia kusambaa zaidi kwa maambukizo hayo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa likisisitiza kuchukuliwa kwa tahadhari ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!