October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Corona: Chadema yaiangukia serikali

Bendera ya Chadema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani kimeiomba serikali kutoa taarifa za kina zaidi juu ya maambukizi ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea). 

Wito huo umetolewa leo tarehe 3 Aprili 2020, Hemed Ally, Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani.

“Tunahitaji uwazi zaidi kuhusu maambukizi ya Corona, kwa Dar es Salaam tunao wagonjwa kumi na hatujui mlolongo wao. Ili tujue kwa kiwango gani na kiasi gani tunaweza kukabiliana nao,” ameshauri Ally.

Ally ameshauri serikali kuanzisha mpango wa dharura utakaohusisha watalaamu wa afya na uchumi ili kukabiliana na janga hilo.

“Inahitaji wadau zaidi. Hili jambo halipo sawasawa. Tunahitaji jopo la watalaamu wa afya na uchumi. Pia kujua hii bajeti ya dharula ya afya itapatikana wapi. Tunahitaji mpango wa dharula unaohusisha wataalamu wa afya na uchumi ili kujSerikaliua tunakabilianaje,” ameshauri Ally.

Wakati huo huo, Ally ameshauri viongozi wa dini kuzuia mikusanyiko ya watu katika maeneo ya ibada, ili kuounguza kasi ya ueneneaji wa COVID-19.

“Viongozi wa dini wadhibiti mikusanyiko mikubwa katika maeneo ya ibada. Waweke watalaamu wa kutoa elimu. Kila mahali inapohitaji elimu, ifikishwe hasa na watalaamu wa afya.Viongozi wa dini watambue Corona iko na inauwa watu wengi,” amesema Ally.

error: Content is protected !!