May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Corona-19: WHO, Tanzania kukaameza moja

Dk. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya wa Tanzania

Spread the love

 

TANZANIA na Shirika la Afya Duniani (WHO), wanatarajia kukaa meza moja ili kuangalia namna ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Vikao hivyo vya kitaaluma vimepangwa kuanza Julai 2021, ambapo tayari serikali imezindua Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Sekta ya Afya (2021-2025) unaotarajiwa kugharimu Sh. 47 trilioni.

Mpango huo ulizinduliwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, jijini Dar es Salaam.

Alisema, katika kukabiliana na wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa huo, Julai 2021 serikali itahusisha vikao vya kitaalamu chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Serikali na Uenyekiti mwenza wa Mwakilishi Mkazi wa WHO.

“Sambamba na kuanza vikao hivyo ninaelekeza vikao vya kila mhimili katika Mpango wa Taifa wa Udhibiti Ugonjwa wa UVIKO-19 vianze kwa lengo la kudhibiti ugonjwa huo nchini,” alisema.

error: Content is protected !!