Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko CoRI waitaka Serikali ya Tanzania kuteua maofisa taarifa
Habari Mchanganyiko

CoRI waitaka Serikali ya Tanzania kuteua maofisa taarifa

Spread the love

 

UMOJA wa asasi zinazotetea haki ya kupata taarifaTanzania (CoRI) umeitaka Serikali ya nchi hiyo kuteua maafisa taarifa katika ofisi zote za umma, kuboresha upatikanaji wa taarifa na kuhakikisha utekelezaji wa sharia unafanyika. Anaripoti Patricia Kighono TUDARCo … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatatu tarehe 27 Septemba, 2021 na umoja huo unaoundwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania (THRDC) na Jamii Forum, Policy Forum na Twaweza.

Wengine ni, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tan) na Kituo cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Sikika.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, katika ofisi za LHRC, Kijitonyama mkoani Dar es Salaam, Mwenyekiti wa umoja huo, Kajubi Mukajanga amesema, katika kuelekea kilele cha siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa, Serikali itekeleze sharia ya haki ya kupata taarifa.

Kajubi ambaye pia ni katibu mtendaji wa MCT amesema, mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) ulitangaza tarehe 28 Septemba ya kila mwaka iwe inaadhimishwa katika nchi wanachama.

“Kipekee, CoRI tunataka kuteuliwa kwa maofisa watoa taarifa katika kila taasisi ya umma wenye mamlaka na wajibu wa utoaji wa taarifa za mara kwa mara na zile zinazoombwa na mwananchi mmoja mmoja kama inavyotamkwa na kifungu cha saba cha sharia,” amesema Kajubi

Pia, amesema, utoaji wa mara kwa mara wa taarifa muhimu pamoja na kuanzishwa kwa mfumo wa ufuatiliaji kubaini maombi yote ya taarifa na majibu yake kutoka ofisi za umma.

“Ni kutokana na ukweli huu, siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa mwaka huu wa 2021, inakuwa fursa kukumbushana juu ya muhimu wa mijadala wa kitafa juu ya namna ya kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa taarifa nchini Tanzania,” amesema

Aidha, Ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania, inatambua na kutamka taarifa ni haki ya kimsingi ya kila mtu ambapo kila mtu ana uhuru wa maoni, kujieleza na kujumuika.

Hata hivyo, umoja huo umekiri kutoridhishwa na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ambapo kupitia mjumbe wake, Anna Rugaba ambaye ni meneja utetezi Twaweza amesema;

“CoRI tunaamini ipo haja ya marekebisho ya Sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016, kuongeza kasi ya utekelezaji wa sheria ya haki ya kupata taarifa pamoja na maboresho na utekelezaji wa kanuni za sheria hizo kama njia ya kuimarisha mfumo wa kitaasisi utakaosaidia kufikiwa kwa uhuru kamili wa habari.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amesema, safari bado ni ndefu katika kufikia lengo la uhuru kamili wa habari kwa kila mtu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!