April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Conservative chaibua mshindi Uingereza

Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza na Kiongozi wa chama cha Conservative

Spread the love

CHAMA cha Conservative cha Uingereza, kimeshinda uchaguzi wa mapema nchini humo. Kimepata viti 364, kutoka 326 ilivyokuwa inavihitaji kutangazwa mshindi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Boris Johnson, waziri mkuu na kiongozi wa chama hicho,  amewashukuru wapiga kura nchini mwake kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi huo. 

Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama chake kutangazwa kushinda zaidi ya viti 326, Jonhson amesema, hatua hiyo inaipatia serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya raia wa Uingereza ili kuliimarisha taifa hilo.

Ameongeza: “Uamuzi huo unampatia jukumu la kufanikisha Brexit na kuiondoa Uingereza katika muungano wa Ulaya.”

Amesema, atafanya kazi usiku na mchana, ili kuwalipa wapiga kura waliomuonyesha uaminifu baada ya kukisadia chama chake cha Conservative kupata ushindi wa kihistoria.

Huku ikiwa imesalia maeneo bunge mawili kutangazwa, chama cha Coservative kina wingi wa viti 76.

Akiungumza jukumu lake kuindoa Uingereza katika muungano wa EU, waziri mkuu alisema: “Raia wanataka mabadiliko. Hatuwezi kuwavunja moyo.”

Hatua hiyo inajiri muda mchache baada ya mpinzani mkuu wa Boris Jonson, kiongozi wa chama cha Leba, Jeremy Corby, kukiri chama chake kushindwa na kusema hatokiongoza tena chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Uamuzi huo wa kiongozi wa Leba unajiri huku chama hicho kikikabiliwa na matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi katika miongo kadhaa.

Chama cha Leba kimepoteza viti kaskazini mwa England, Midlands na Wales, yakiwa ni maeneo yaliopiga kura ya Brexit katika kura ya maoni ya mwaka 2016.

Leba kinatarajiwa kushinda viti 61 ikiwa ni chini ya viti ilivyoshinda mwaka 2017.

Baadhi ya maeneo Bunge kama vile Darlington ama Workington, kaskazini mwa England yataongozwa na mbunge wa Chama cha Conservative kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa- ama katika matukio ya Bishop Auckland na Blyth Vally kwa mara ya kwanza tangu viti hivyo kubuniwa.

Lakini Leba kimeshinda kiti cha eneo Bunge la Putney, Kusini Magharibi mwa London kutoka kwa Conservative.

Chama cha Uskochi cha kitaifa kimepata ushindi wake wa kwanza usiku wa kura; kikishinda eneo bunge la Rutherglen na Hamilton Magharibi kutoka kwa chama cha Leba na Angus kutoka kwa Conservative.

Boris Johnson, alimrithi Theresa May, kama kiongozi wa chama cha Conservative baada ya mwanamama huyo kuamua kuachia ngazi.

Alipoingia kwenye ofisi ya waziri mkuu kwa mara ya kwanza, wakosoaji wake walidai Boris hakuwa chaguo la watu wa Uingereza.

Kwa mujibu wa taratibu za demokrasia ya Uingereza, kiongozi wa chama chenye uwakilishi mkubwa bungeni huwa waziri mkuu, na hivyo baada ya kupigiwa kura za chama, Boris akashika uongozi wa wa Uingereza.

Lakini katika uchaguzi wa jana Alhamisi ambao matokeo yake yamewekwa bayana leo Ijumaa, wamepaza sauti zao juu ya Boris, baada ya kukipa ushindi chama cha Conservative kwenye uchaguzi huo.

Kufuatia maamuzi hayo, Boris ametengeneza jina lake kwa kugawa mawazo ya watu na kuchochea migongano, awali akiwa mwanahabari na baadae mwanasiasa.

Baada ya kuchukua hatamu za uongozi wa chama, wengi walimbeza kuwa hana ujuzi wa kutosha wa kukiongoza chama.

Lakini, matokeo haya sasa yanaonesha hali ya tofauti. Swali ni amefikaje hapa alipo?

Tokea mwanzo, Boris amejipambanua kama mtu mwenye mashaka na Muungano wa Ulaya.

Alizaliwa jijini New York baba yake akiwa mwanadiplomasia na mama yake msanii. Babu yake mkuu alikuwa ni mwandishi wa habari wa Kituruki.

Amekulia Marekani, Uingereza na Ubelgiji kabla ya familia yake kurejea rasmi nchini Uingereza.

Amesoma Eton, shule maarufu zaidi ya wavulana nchini Uingereza, na huko ndipo dalili za tabia na mtu gani angekuwa zilianza kuonekana.

Kutoka hapo akaenda Chuo Kikuu cha Oxford, na kuchaguliwa kuwa rais wa chama cha midahalo cha chuo hicho.

Johnson alifukuzwa Times lakini baadae alipata ajira The Daily Telegraph na The Spectator. Tabia yake ya kuchochea malumbano ilionekana wazi akiwa mwandishi.

Alitimuliwa kazi katika gazeti la The Times baada ya kughushi nukuu.

Baada ya hapo akaajiriwa kama ripota wa jijini Brussels wa gazeti linaloogemea mrengo wa chama cha Conservative la The Daily Telegraph.

“Uandishi wake ulichanganya kwa umaridadi uhalisia na mambo ya kubuni dhidi ya Umoja wa Ulaya,” anaeleza mhariri msaidizi wa BBC wa habari za siasa, John Pienaar.

Anasema, habari alizoandika zilizaa mjadala mkubwa na mashambulizi dhidi ya Umoja wa Ulaya ambayo baadae alikuja kuyaendeleza kama mwanasiasa.

Lakini baadhi ya waandishi wenzake walimtuhumu kwa kutokuwa mwaminifu kwa taaluma yake.

Hapo awali nchini Uingereza alikuwa mwandishi wa makala katika gazeti la The Telegraph na baadae mhariri wa gazeti la mrengo wa kulia, The spectator.

Johnson alionesha mwelekeo wa kuwakosea baadhi ya wasomaji, kwa kutumia maneno ya kejeli kuwaelezea watu weusi na kuwaita watoto wanaolelewa na mama mzazi peke yake kama ”watoto ambao hawajelelewa vizuri, wajinga, wenye fujo, na wasio halali.”

Lakini aliliongezea mashabiki gazeti hilo na wasifu wake katika vyombo vya habari ukakua na akaanza kuonekana katika kipindi cha kila siku kiitwacho ”Have I Got News For You?” ambacho washiriki hujaribu kufanya ucheshi kuhusu habari za wiki.

Kama maneno na maoni yake yalivutia ukosoaji, basi pia yalimfanya awe mtu maarufu katika siasa, kulingana na maneno ya watoa maoni wengi akiwemo aliyemwandikia historia ya maisha yake, Sonia Purnell. Na hiki ndicho kilichomsaidia kwenye mwanzo wake katika siasa.

Mwaka 2001, Johnson alikuwa Mbunge, akikiwakilisha chama cha Conservative katika wilaya ya Henley-on-Thames, karibu na Oxford.

Katika uchaguzi wa mwaka 2007 kama meya wa London ndio uliompaisha kwa kasi kubwa katika jukwaa linalojulikana ulimwenguni.

Wakati macho yote duniani yakiiangalia mji ambao ulikuwa mwenyeji wa mashindano ya olimpiki ya mwaka 2012, Jonson alikuwa balozi wa michezo hiyo, ingawaje hayakuandaliawa na City Hall.

Moja ya programu zake maarufu za usafiri alizozianzisha, ni uliojulikana kama mpango wa kuendesha baiskeli ”Boris Bike”, na ulianzishwa mwezi Julai mwaka 2010.

Ni ushahidi tosha wa nafasi yake iliyochanganyika siasa na umaarufu wake, ambao umemfanya ajulikane kama Boris.

Siku zote Johnson alipigia debe baiskeli hizo kwa kuziendesha yeye mwenyewe, huku mara moja alionekana akiwa na muigizaji mkongwe wa Hollywood, Arnold Schwarzenegger.

Wakosoaji wanadai haukuwa mpango wake ila mpango wa meya aliyopita.

Malengo makubwa ya kutaka kutengeneza daraja la bustani juu ya mto Thames ikiwa kama kumbukumbu ya binti wa kifalme Diana, yalifutwa na mrithi wake, Sadiq Khan, baada ya dola milioni 70 kutumika.

Lakini wakati Johnson akiwa amerudi bungeni baada ya kushinda kiti katika uchaguzi wa mwaka 2015, na mbele ya kura za maoni za Brexit, msimamo wa Johson katika swala hili ulikuwa bado haueleweki.

Aliandika nakala katika gazeti akiitaka Uingereza iondoke Umoja wa Ulaya na akaandika nakala nyingine anayoitaka Uingereza ibaki katika Umoja wa Ulaya.

Lakini alikuja kuamua kuunga mkono hoja ya Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya, kitendo kilichomfanya kwenda kinyume na kiongozi wa chama chake, waziri mkuu David Cameron.

Baada ya ushindi wa kutaka Uingereza kutoka umoja wa ulaya na Cameron kujiuzulu, Johnson aliweka wazi malengo yake ya kutaka kuchukua nafasi yake kama kiongozi wa chama cha Conservative.

Lakini Theresa May aliweza kuibuka mshindi badala yake, na wagombea wengine wote walijitoa kugombea nafasi hiyo kabla ya upigaji kura kuanza.

Hata hivyo, kama shukran kwa Johnson kwa ajili ya nafasi yake kama bingwa wa Brexit, akateuliwa kuwa kama katibu wa mabo ya nje.

Wakati wa kampeni za Brexit, jina la Johnson lilihusishwa na madai kuwa kuondoka umoja wa ulaya kutaruhusu paundi milioni 350 kwa ajili ya shirika la afya la taifa, kila wiki. Hilo halikumchafua kwa watu waliounga mkono Brexit.

Johnson na viongozi wengine wa-Brexit walidai kuwa Brexit inaweza kutoa $460m kwa wiki kwa ajili ya huduma ya afya

Na baadaye Johnson aliamua kuondoka katika baraza la May akidai kuwa anahitaji kuwa shupavu katika mazungumzo na Brussels.

Tangu kiongozi wa chama hicho, na hata waziri mkuu, Johnson hajawahi kukubali kuondoka umoja wa ulaya bila makubaliano yoyote.

Amesema kama Conservatives wakishinda uchaguzi mkuu, Uingereza itaondoka ifikapo tarehe 21 Januari 2020.

Katika Brexit ya Uingereza, maoni na vinaweza kuwashawishi wapiga kura.

Katika maisha yake, Johnson ameonesha uwezo wa kiwango cha juu.

error: Content is protected !!