Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu CoNAS yajivunia kutoa watafiti wengi wa sayansi asilia nchini
ElimuHabari

CoNAS yajivunia kutoa watafiti wengi wa sayansi asilia nchini

Spread the love

KATIKA kutimiza miaka 60 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi inajivunia kutoa wataalum wengi wa Sayansi Asilia ambapo kupitia ujuzi wao wameweza kufanya tafiti mbalimbali zilizoleta tija nchini katika miaka yote ya kutoa huduma yao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hayo yamebainishwa hii leo Jumatano tarehe 22 Juni, 2022, na mkuu wa ndaki hivo Prof. Frola Magige katika hafla ya kusheherekea miaka 60 ya utoaji wa huduma wa chuo hicho kikongwe nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Prof Magige amesema kuwa, wanachojivunia mpaka sasa kama ndaki ni kuongeza idadi kubwa ya watafiti, ambao wamekwenda kuisaidia jamii kupitia tafiti zao.

“Tunajivunia mengi kwa kuongeza idadi ya watafiti ambapo kupitia tafiti zao zimekwenda kuisadia jamii” amesema Prof. Magige

Ameendelea kwa kusema kuwa moja ya tafiti kubwa walioifanya katika kipindi cha hivi karibuni, ni kuvumbua dawa ambazo zinasaidia kufubaza virusi vya UVIKO 19, ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia watu waliokumbwa na maradhi hayo.

“Tafiti tuliyofanya yenye manufaa ni uvumbuzi wa dawa ya UVIKO 19 ambayo inaitwa Yudano ambayo imesaidia watu wengi kupona, na mpaka sasa bado inaendelea kuuzwa,” amesema Mkuu huyo.

Amehitimisha kwa kusema kuwa, Watanzania watarajie mambo makubwa kutoka kwenye ndaki hiyo kwa uvumbuzi wa mambo mbalimbali.

“Tutarajie kuona mambo makubwa kutoka kwenye ndaki hii, kwa kuwa ubunifu unaendelea na maandiko yanaendelea ambayo yataleta uvumbuzi wa mambo mbalimbali,” amesema.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Shahada za awali, Prof. Nelson Boniface, ambaye alihudhuria hafla hiyo kumuwakilisha makamu Mkuu wa chuo hiko Prof. Willium Anangisye, aliwatia moyo ndaki hiyo na kuitaka kujikita kwenye tafiti ambazo zitasaidia jamii ya Watanzania.

“Makamu Mkuu wa Chuo amenituma kuwatia moyo wana CoNAS sambamba na kuwataka kufanya tafiti ambazo zitasaidia jamiii ya watanzania na kuelenga ajenda ya Taifa,” amesema Prof. Boniface.

Chuo hiko kimetimiza miaka 60, tarehe 21 Oktoba 2021 toka kilipoanza rasmi kutoa huduma zake Oktoba 1961.

https://www.youtube.com/watch?v=tc9eAj5lpjw

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!