MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amesema, amepata wadau waliokubali kuwajengea wafanyabiashara wa ufukwe wa Coco vibanda vya kisasa na kuboresha mandhari ya ufukwe huo ili uwe kwenye mwonekano wa kisasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
RC Makalla amesema hayo leo Jumanne, tarehe 24 Agosti 2021, alipotembelea ufukwe huo akiambatana na viongozi na wadau waliokubali kuwa sehemu ya maboresho ya fukwe wakiwemo Bank za NMB, CRDB, Kampuni za utengenezaji wa Vinywaji zikiwemo TBL, Coca-Cola, Pepsi, Asas na Azam group.
Amesema wa dhamira yake na Serikali ni kuona Coco inakuwa ya kisasa na shughuli za kiutalii zinafanyika ambapo tayari amezungumza na Mfanyabiashara mkubwa nchini Said Salim Bakhresa kwaajili ya kuleta boti za utalii kwenye fukwe hiyo.
Aidha RC Makalla ameelekeza Manispaa ya Kinondoni kuanza mara moja Ujenzi wa Ofisi, Stoo na vyoo vya kisasa kwenye ufukwe huo.
Hata hivyo, Makalla ametoa maelekezo kwa Manispaa ya Kinondoni kupeleka umeme eneo lote la Coco huku akimuelekeza Kamanda wa Polisi Kinondoni kuimarisha ulinzi kwenye ufukwe huo.
Mpango wa RC Makalla kuboresha fukwe za Dar es Salaam unaenda sambamba na maboresho ya maeneo ya wazi, ustani za kupumzika, usafi na upandaji wa miti, maua na kinbgo pembezoni mwa Barabara.
Leave a comment