December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Coaster lagonga lori sita wafariki papo hapo

Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wankyo Nyigesa (katikati)

Spread the love

WATU sita wamepoteza maisha huku saba wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria iliyotokea leo tarehe 6 Novemba 2018 maeneo ya Segera mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kuhusu ajali hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wankyo Nyigesa amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la abiria aina ya Coaster lenye namba za usajili T124 DHW kugonga kwa nyuma lori lililoegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo.

Kamanda Wankyo amesema lori hilo lenye usajili wa namba za nchi jirani, liliegeshwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo katika barabara ya Segera.

Aidha, Kamanda Wankyo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Bagamoyo.

error: Content is protected !!