May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Coastal Union yashusha kocha Mmarekani

Melis Medo

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Coastal Union imemtambulisha Kocha wake mpya, Melis Medo kwa mkataba wa miaka miwili, leo tarehe 30 Agosti, 2021 kupitia mtandao wake wa kijamii wa instagram. Anaripoti Wiston Josia TUDARCo … (endelea).

Klabu yenye makao makuu yake jijini Tanga, imemtambulisha kocha huyo kwa lengo la kuimarisha kikosi chake ambacho katika msimu uliopita hakikufanya, hali iliyopelekea kuchezwa katika hatua ya mtoano ili kubali Ligi Kuu msimu.

Coastal iliyokuwa inanolewa na Juma Mgunda, katika hatua hiyo walikutana na Pamba ya Mwanza na kufanikiwa kushinda na kubaki katika ligi hiyo.

Medo raia wa Marekani, alikuwa anaifundisha timu ya Gwambina FC ya Misungwi jijini Mwanza.

Coastal imelazimika kufanya mabadiliko hayo ya benchi la ufundi kwa lengo la kujiweka vizuri karika msimu huu na kuepuka kile kilichotokea msimu uliopita kunusulika kushuka daraja.

error: Content is protected !!