August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Clinton na Sanders watoleana uvivu

Spread the love

WAGOMBEA wa Demokrati Hillary Clinton na Bernie Sanders wametoleana na uvivu kwa majibizano makali katka mdahalo ulio fanyika katika jiji la New York huku kila mmoja akitilia shaka uwezo wa mwenzake, anaandika Wolfram Mwalongo.

Wagombea hao wawili ndio waliosalia wanaowania kuteuliwa na chama hicho katika kinyang’anyiro cha Urais.

Katika mdahalo huo walionyesha kutokuaminia na hasa katika kusimamia udhibiti umiliki wa silaha na mishahara ya wafanyakazi kwa taifa hilo ambapo Sanders amemkosoa Bi Clinton kwa kuunga vita vya Iraq na kutetea mikataba ya biashara huru.

Kwa upande wake Bi Clinton amemtuhumu Sanders kuwa hawezi kutekeleza hata sera zake mwenyewe pamoja na kuvunja udhibiti wa benki kuu za Wall Street.

Wagombea hao wote maarufu katika jimbo la New York ambapo Sanders ni mzaliwa wa jimbo hilo na Bi Clinton amekuwa Seneta wa jimbo hilo kwa miaka nane.

Hadi sasa Sanders ameshinda majimbo saba kati ya nane jambao ambalo linapunguza kasi ya uongozi wa Clinton katika mchujo wa chama lakini Clinton anajivunia nguvu ya uongozi aliyo nayo kutoka kwa chama kilichoko madarakani.

error: Content is protected !!