Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Chuo cha Kilimo cha Mwl. Nyerere kuanza kutoa mafunzo mwaka huu
Elimu

Chuo cha Kilimo cha Mwl. Nyerere kuanza kutoa mafunzo mwaka huu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
Spread the love

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amekitaka Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) kilichopo Butiama mkoani Mara kujikita kutoa mafunzo kwenye eneo la kilimo kwa upana wake ambao ndio msingi halisi wa uanzishwaji wa chuo hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara… (endelea).

Prof. Mkenda ameyasema hayo Wilayani Butiama alipotembelea chuo hicho na kuwataka kuhakikisha kuwa pamoja na mafunzo wanafanya tafiti na kusambaza matokeo ya tafiti hizo ili kunuifaisha wakulima kwa kuongeza tija na uzalishaji.

Waziri Mkenda ameeleza kuwa chuo hicho kitaanza rasmi kutoa mafunzo mwaka huu 2023 na kuagiza uongozi wa chuo kuhakikisha matayarisho yote yanakamilika.

Amesema mkakati mbalimbali itatumika kuhakikisha wanafikia vigezo vya kupata ithibati ili kuruhusu kutoa mafunzo ikiwemo kuongeza wanataauma na kuweka mazingira na miundo mbinu stahiki ya kufundishia na kujifunzia.

“Tutahakikisha MJNUAT Butiama kinaanza kutoa Mafunzo mwaka huu 2023 tayari Serikali imetoa Shilingi bilioni 2.6 kwa ajili ya kukarabati majengo yaliyopo na kujenga hosteli mpya 2 ili wanafunzi watakapoingia wakae katika mazingira bora ,” amefafanua Waziri Mkenda.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda

Profesa Mkenda ameongeza kuwa Serikali pia imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 102 kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa mageuzi ya Kiuchumu (HEET) kwa ajili ya kujenga makao makuu ya Chuo hicho hapo hapo Butiama.

Amesisitiza kuwa uwepo wa MJNUAT ni moja ya njia za kuenzi maono ya Baba wa Taifa kuhusu kutoa elimu ujuzi ikiwemo elimu ya kilimo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mosses Kaegele ameishukuru Serikali kwa kuendeleza Ujenzi wa Chuo Kikuu cha MJNUAT na kuhakikisha kinakwenda kuanza kutoa mafunzo mwaka huu.

“Tunapongeza sana kwa hatua hii ya Wizara kuhakikisha Chuo kinaanza udahili . Na katika kazi ya ukarabati Katika Wilaya tunauzoefu na kazi za ujenzi kupitia mfumo wa  Force account tutsaidia kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora ili thamani ya pesa ionekane,” ameongeza Kaegele.

Jumanne Sagini, Mbunge wa Butiama ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kutoa fedha kukiendeleza Chuo cha MJNUAT kuhakikisha sasa kinakwenda kuanza kutoa mafunzo, kuunda Baraza, kuteua Mwenyekiti na Mkuu wa Chuo.

“Napongeza pia mtazamo wa Wizara kuhusu mafunzo kuhakikisha yanajenga ujuzi. Hii ni inaashiria kuwa vijana wakitoka hapo MJNUAT wataweza kujiajiri katika kilimo,” ameongeza Sagini.

Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa chuo cha MJNUAT, Prof. Lesakit Mellau amesema chuo hicho kinaendeshwa kwa usajili wa muda ‘provisional registration license’ na kwamba kilianza rasmi Machi 2015 baada ya Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete kuteua viongozi.

Amesema kuwa tayari wameshaandaa mitaala 29 ikiwemo 20 ya Shahada ya Awali na 9 ya Diploma na kuongeza kuwa udahili unaotarajia kuanza baadae mwaka huu utaanza na wanafunzi 400.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

error: Content is protected !!