August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chungu ya Lema kwa Magufuli hii hapa

Spread the love
HOFU ya Mussa Azzan Zungu, Mwenyekiti wa Bunge kuruhusu Hotuba ya Godbless Lema, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni pamoja na maneno yaliyotumika kwenye hotuba hiyo, anaandika Faki Sosi.
Pamoja na vipengele vingine Bunge limedai kwamba, maneno yaliyotumika kwenye hotuba hiyo kuhusu tabia ya Rais John Magufuli hayafai. Ifuatayo ni sehemu ya  hotuba ya Lema katika kipengele hicho.
6.3 Tabia ya Rais Magufuli na Usalama wa Nchi.
Mheshimiwa Spika, wakati Taifa letu linapita kwenye changamoto nyingi Kama vile ukosefu wa sukari, umeme, umasikini, mizigo kupungua bandarini, madini ya Tanzanite kuanguka bei na ubadhirifu uliokithiri katika mfumo wa utawala. Rais mwenyewe ameonekana kufuatilia na kufanyia kazi habari za kwenye mitandao ya kijamii.
 Kwa tabia hii ya Rais Magufuli, kama Taifa tunahitaji maombi haraka, kwani Rais ataumiza  watu wengi  sana kwa kufuatilia  maneno ya mitaani kwa njia mbali mbali , kwani kwa madaraka  aliyonayo  Rais bila shaka ataumiza watu wengi. Mfano, Sakata la Mke wa Waziri Mahiga na Trafiki barabarani. Ni jambo dogo sana na la karaha kuona linazingatiwa na Rais .
Mheshimiwa Spika, haikuwa  busara Rais kukemea familia ya Waziri wake mbele ya vyombo vya habari na kuagiza askari huyu kupandishwa cheo bila kujua historia ya utumishi wake .
Mheshimiwa Spika , kwa nini mambo haya ni muhimu kuyasema na kwa nini ni hatarishi kwa usalama wa Nchi, tulipoonza vikao vya Kamati za Bunge, vyombo vya habari vilimnukuu Rais akielezea mpango wake wa kuanza kurekodi Mawaziri wake wanaolalamika juu ya staili yake ya uongozi. Kwa hiyo leo ukienda kwenye ofisi za Mawaziri, unaona, hofu, mashaka, kutokujiamini, mambo yatakayo punguza ufanisi, ubunifu na uhuru katika utendaji wao, jambo linalopeleka Taifa kuzorota katika Nyanja zote kwa utumishi wa umma jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.
error: Content is protected !!