January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chozi la Kingunge kwa Lowassa halikauki

Kingunge Ngombare Mwiru (kushoto) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa

Spread the love

CHOZI la kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) halitakauka, ni kwa kuwa ‘tumaini lake’ katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu ndani ya chama hicho limeyeyuka. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Jana mbele ya waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Kingunge amendeleza kilio chake kwa kukituhumu chama chake kwamba, ‘kimekiuka kanuni na taratibu za mchakato wa uteuzi kwa mgombea urais wa CCM.’

Kauli ya Kingunge imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kukatwa kabla ya jina lake kupelekwa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC- CCM) kupigiwa kura.

Majina yaliyongia kwenye hatua hiyo ni Asha-Rose Migiro, Dk. John Magufuli, Balozi Amina Salum Ali, January Makamba na Bernard Membe.

Kingunge ambaye amejitambulisha kuwa mfuasi wa Lowassa ameelekeza shutuma hizo kwa Kamati ya Maadili ya CCM kutokana na kumwengua Lowassa.

Katika kuonesha hasira zake dhidi ya Kamati ya Maadili Kingunge aliishambuliwa kwamba, inajipamba kwa kuitwa jina hilo wakati haina maadili, “wanajiita Kamati ya Maadili wakati yenyewe haina maadili.”

Hatua ya kukatwa kwa Lowassa ilimfikirisha Kingunge na kufikia hatua ya kuhoji upole wa Watanzania na kushindwa kuhoji baadhi ya mambo ndani ya nchi yao.

Hata hivyo Kingunge amesema, “CCM si chama kipya, kina katiba, taratibu na wajibu mzuri wa kupata viongozi, siasa ni suala la watu linahusu hatma yao. Hivyo wanaonesha mapenzi na matarajio kwa wagombea wanaowaamini.” 

Tangu hekaheka za uteuzi ndani ya CCM kuanza, Kingunge amekuwa miongoni mwa makada wa chama hicho aliyejitowa waziwazi kumpigania Lowassa katika safari yake ya matumaini.

Jumamosi ya Mei 30 mwaka huu, Lowassa alijitokeza mbele ya wananchi katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuelezea nia yake ya kuomba kuteuliwa na chama chake kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Katika mkutano huo, ni Kingunge pekee ndiye aliyetumia muda mrefu katika kumpamba Lowassa.

error: Content is protected !!