Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo awatahadharisha wana-CCM waliopewa dhamana na wananchi
Habari za Siasa

Chongolo awatahadharisha wana-CCM waliopewa dhamana na wananchi

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo
Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Danieli Chongolo, amewatahadharisha wanachama wa chama hicho ambao walipata dhamana ya uongozi wa Serikali za Mitaa lakini hawatimizi majukumu yao na kusababisha wananchi kuichukia. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Chongolo ametoa tahadhari hiyo leo Jumanne tarehe 24 Januari, 2023, wakati wa kuitambulisha Sekretarieti kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika makao makuu ya CCM Jijini Dodoma.

Chongolo amewataka kila mmoja atimize wajibu wake ili kuepukana na chuki hiyo ambayo inaweza kuwasababishia wananchi kuwauliza maswali mengi wakati wa kuendelea kutafuta dola na kushika dola.

“Chama chochote cha siasa kazi yake kutafuta na kushika dola sasa tuna kazi ya kusimamamia dola tuliyopewa na dhamana ya kuishika na wananchi ili ifikapo 2025 tusiende kuulizwa maswali na wananchi,” amesema Chongolo.

“Ndugu zangu 2019 chama kilipewa dhamani ya kushika nafasi za serikali za mitaa wajibu huo unatakiwa kuusimamia ili tuendelee kuaminiwa zaidi na zaidi ndugu zangu wajibu huo si wakukaa, kilegelege, wala kuzembea;

“Mkoa badala ya kutimiza wajibu wake anakaa analalamika hayupo kwenye wajibu wa kusikiliza malalamiko ya watu bali yupo kwenye kulaumu, utamkuta Waziri aliyepewa wajibu na majukumu ya kufanya kazi na kupewa dhanana ya kuwatumikia watu anashindwa kutumikia badala yake anachelewesha maendeleo,” amesema Chongolo.

Aidha Chongolo amewakemea baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwa kuendeleza malalamiko badala ya kufanya kazi kwa kutimiza majukumu yao.

Mbali na kuwakemea Viongozi hao amewatangazia kihama viongozi hao ambao wanatumia muda mwingi kulalamika na kwamba kulalamika kwao kunaonesha wazi kuwa hawatoshi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!