Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the love

KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amesema ipo haja ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kutembelea na kutatua mgogoro wa mradi wa umwagiliaji wa Luhindo wenye thamani ya sh mil 900.1 ambao licha ya kukamilika miaka mitatu iliyopita bado haijaanza kufanya kazi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Chongolo alisema hayo akiwa Wilayani Mvomero mkoani hapa kwenye ziara yake ya siku 9 ambapo alisema haiwezekani Serikali ikatoa fedha nyingi katika kukamilisha miradi ya maendeleo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi huku bado mradi usifanye kazi na kuondoa maana aliyoitaka Rais Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo nchini.

Aidha amewataka viongozi wote wa serikali kuanzia ngazi ya vijiji  kuzingatia miiko ya uongozi ili kukabiliana na migogoro ya ardhi inayoendelea kuchipua katika baadhi ya maeneo nchini.

Akizungumzia changamoto ya umeme wa Wakala wa nishati vijijini ( REA) kwa vijiji 60  aliagiza mkandarasi kampuni ya HNXJDL INT Contructirs kuhakikisha wanafika angalau asilimia 80 ya ujenzi ifikapo mwezi Februali mwaka huu au kukamilisha ujenzi huo vinginevyo atasimamishwa kuendelea na ujenzi huo kupisha wakandarasi wengine.

Hata hivyo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Dk. Philiphine Titus kutengeneza mpango mkakati utakaoonesha gharama halisi za ujenzi na umuhimu ili kuona haja ya kuanza ujenzi wa soko la Mpunga katika Wilaya hiyo.

Awali Mbunge wa jimbo la Mvomero Jonas Van Zeeland alimshkuru Rais Samia kwa kuwasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali kwenye wilaya hiyo licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa zinazowakabili wananchi wa Wilaya hiyo.

Alizitaja changamoto zinazowakabili eneo la Dakawa ni pamoja na upatikanaji wa maji ya Bomba, kukamilika kwa Zahanati ya Kijiji na migogoro ya mipaka baina ya vijiji na vijiji

Akiwa katika shina namba 18 kwenye Kijiji hicho akipokea jumla ya wanachama 13 wapya waliojiunga CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!