Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo aonya wanaopanga uongozi CCM 2022
Habari za SiasaTangulizi

Chongolo aonya wanaopanga uongozi CCM 2022

Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amewaonya wanachama wa chama hicho, walioanza kupanga safu za uongozi kuacha mara moja. Anaripoti Matrida Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Ni katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho, utakaofanyika mwaka 2022.

Chongolo, ametoa marufuku hiyo leo Jumamosi, tarehe 22 Mei 2021, ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, alipokuwa anazungumza na wanachama wa chama hicho, waliojitokeza kuwapokea viongozi wa sekretarieti nzima, ambayo anaiongoza yeye.

“Mwakani tutakuwa na uchaguzi wa ndani wa chama, lakini kuna watu badala ya kuhangaika kutekeleza ilani ya chama, watu wanahangaika kupanga safu ya uongozi,” amesema Chongolo

“Wanasema hapa kwa fulani, pale kwa fulani, acheni tabia ya kupanga safu za uongozi na inatusababishia kupata viongozi wa hovyo. Lakini kama hamuamini, muda utasema,” amesema Chongolo ambaye ameteuliwa tarehe 30 Aprili 2021, kushika wadhifa huo.

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM

Amechukua nafasi ya Dk. Bashiru Ally, the ambaye sasa ni mbunge wa kuteuliwa. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Chongo amesema “niwahakikishie, sektretarieti yangu na kamati zote zinazosimamia hili, zitakuwa timamua. Kwa ambao hawaamini, muda ni shahidi mzuri. Chama hiki si chama cha kugawa nafasi.”

Amegusia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 akisema “ni aibu sana tumemaliza uchaguzi mkuu kama miaka miwili iliyopita, watu wameanza kujipanga kuwa wabunge au madiwani. Wacha watu wafanye kazi muda bado.”

“Lazima viongozi wa chama hiki, tujiepushe na migogoro isiyo na sababu, lazima tuhakikishe serikali yetu inatimiza majukumu yetu. Tukibaki sisi tuna nyoosheana vidole hatutafika. Kama huwezi kusimama kwenye nafasi yako, tutakusaidia kumweka mwenzio akusaidie,” amesema Chongolo.

Chongolo amesema “tukiona mnasutana, mnasuguana, sisi tutachukua nafasi.”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!