May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chongolo amrithi Dk. Bashiru CCM, Shaka…

Daniel Chongolo katibu mkuu wa Ccm

Spread the love

 

DANIEL Chongolo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, amethibitishwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Chongolo, amethibitishwa leo Ijumaa, tarehe 30 Aprili 2021, baada ya jina lake, kuwasilishwa na Mwenyekiti mpya wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu wa Itikadi na uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka

Chongolo ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, anachukua nafasi ya Dk. Bashiru Ally, aliyeiacha tarehe 26 Februari 2021, baada ya kuteuliwa na Hayati Rais John Magufuli, kuwa katibu mkuu kiongozi.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally

Pia, kikao hicho cha Halmashauri Kuu, kimemteua, Shaka Hamidu Shaka, kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi.

Shaka aliyewahi kuwa kaimu katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), anachukua nafasi ya Humphrey Polepole, ambaye kwa sasa ni mbunge wa kuteuliwa.

Shaka, alikuwa katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, alisimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa za kumpata Meya wa Manispaa ya Morogoro.

Tuhuma hizo, zilitolewa hadharani na Hayati Magufuli, tarehe 11 Februari 2021, wakati anazindua Soko Kuu la Mkoa wa Morogoro.

Pia, Halmashauri Kuu hiyo chini ya mwenyekiti wake, Rais Samia, imemteua Christina Mdeme, kuwa naibu katibu mkuu wa CCM- Bara, akichukua nafasi ya Rodrick Mpogolo.

error: Content is protected !!