KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemtaka Mbunge wa Itilima, Njelu Silanga kuwawezesha wakulima wa jimbo hilo kuhakikisha kila tarafa wanapata mashine ya kukamua mafuta ya alizeti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu … (endelea).
Lengo ni kuongeza thamani ya zao hilo ambalo kwa Mkoa wa Simiyu, Itilima inaongoza kwa uzalishaji wa alizeti
“Najua Mbunge wenu ana wajibu wa kuwasaidia mashine za kuchuja mafuta ya alizeti, wasaidie wananchi hawa wapate mashine za kuchuja mafuta ya alizeti angalau kwa mashine moja kwa kila tarafa na hili litawasaidia sana kuongeza thamani ya zao hili.”
Chongolo ametoa maagizo hayo kwa Silanga leo Alhamisi tarehe 2 Juni 2022, alipowasili Wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu wakati akiendelea na ziara yake yenye lengo la kukahamasisha uhai wa chama ngazi za mashina na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katibu mkuu huyo alisema kitendo cha kufunga mashine, wakulima wataanza kuuza mafuta badala ya kuuza alizeti zenyewe, ambapo kwa sasa mafuta ya alizeti ndio mafuta bora na ghali zaidi, hivyo wananchi watapata fedha za kutosha tofauti na sasa.
Katibu mkuu anatoa maagizo kwa mbunge? Kwani mbunge anawajibika kwa KM? Makubwa haya