Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo alia na vigingi misamaha ya kodi miradi ya kimkakati
Habari za Siasa

Chongolo alia na vigingi misamaha ya kodi miradi ya kimkakati

Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amesema vigingi vilivyowekwa kwenye misamaha ya kodi ndio kikwazo kikubwa kinachosababisha kuchelewa kukamilika kwa wakati baadhi ya miradi ya maendeleo na kimkakati inayoendelea kutekelezwa hapa nchini. Anaripoti Christina Haule, Kilombero … (endelea).

Amesema kutokana na changamoto hiyo, ipo haja ya kuwepo kwa dirisha moja ambalo litakuwa linawajibika na miradi inayoingia nchini ambayo inahitaji kutekelezwa kupitia msamaha wa kodi, hiyo ni baada ya kushindwa kukamilika kwa wakati ujenzi wa daraja la Ruaha Mkuu linalounganisha Mikumi na Kilombero kutokana na vikwazo vya msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani VAT.

Chongolo ametoa kauli hiyo wakati akiwa Ifakara, wilayani Kilombero mkoani Morogoro ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tisa inayolenga kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 pamoja na kuzungumza na makundi mbali mbali ya kijamii.

“Serikali ni moja, msamaha wa kodi tunatoa wenyewe, mradi tuna sainisha wenyewe, halafu jambo moja la msamaha wa kodi linakuwa nyuma wakati la kusaini mradi linakuwa mbele, ninadhani ifike mwisho na isiwe hoja tena kwa wananchi” amesema Chongolo.

Chongolo ameongeza kuwa kuanzia sasa Serikali inapaswa kuweka mfumo wa kuhakikisha msamaha wa kodi hauwi kikwazo tena kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Mpaka inaitwa msamaha wa kodi maana yake ndani ya Serikali kumechakatwa mradi, tukakubaliana kwamba mradi utatekelezwa kwa kuondosha kodi na hasa ya Ongezeko la Thamani, kwa hiyo lazima twende tukashughulike na hilo” amesisitiza Chongolo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!