Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo akunjua makucha migogoro madiwani, wakurugenzi
Habari za SiasaTangulizi

Chongolo akunjua makucha migogoro madiwani, wakurugenzi

Spread the love

 

BAADA ya kuibuka mivutano baina ya madiwani na watendaji, katika Manispaa za Ubungo na Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeagiza waliosababisha migogoro hiyo wachukuliwe hatua. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo Alhamisi tarehe 20 Mei 2021, jijini Dodoma na Katibu Mkuu CCM, Daniel Chongolo, akizungumzia mivutano hiyo iliyojitokeza hivi karibuni.

Katibu Mkuu huyo wa CCM ameagiza Kamati za Siasa za Mikoa, kuwachukulia hatua watakaobainika kuwa chanzo cha migogoro hiyo.

“Naelekeza Kamati za Siasa na Uongozi wa chama kwenye ngazi husika, kuhakikisha zinajikita kuchukua hatua kwa wale wanaobainika kuwa chanzo cha chokochoko. Hatuko tayari kuona chokochoko hizi zikiendelea,” amesema Chongolo.

Mwanasiasa huyo amewaonya madiwani wa chama hicho na watendaji wa halmashauri, kuacha mara moja vitendo hivyo, akisema kwamba, watakaobainika kuhusika watakuwa wamepoteza nafasi zao.

“Nimeona kumeanza kuibuka vitendo vya baadhi ya baraza la madiwani na watendaji kunyukana hadharani na kuonesha tofauti zao, hili jambo halikubaliki. Nitoe onyo kwa wale wataothibitika kuwa vinara wa uchochezi na uanzishaji vurugu kwenye maeneo mbalimbali,” amesema Chongolo.

Katibu Mkuu mpya huyo wa CCM amesema “mtu yeyote atakayetukwaza tutamuweka pembeni katika chama hiki, maana yake hao wameshindwa kutendea haki dhamana zao.”

Aidha, Chongolo amewataka viongozi hao kutumia njia sahihi katika kutatua migogoro yao, badala ya kuianika hadharani, kitendo kinachochafua CCM.

“Tunategemea mabaraza ya madiwani yamepewa dhima kubwa, na watendaji kwenye halmashauri zetu wamepewa dhamana kubwa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji ilani kwenye maeneo yao. Tabia ya kuanza kunyoosheana vidole, kuvutana na wengine wanasema kuumbuana sio tabia ya kiuungwana,” amesema Chongolo na kuongeza:

“Tuna mifumo yetu ya ndani ya kumaliza changamoto kwenye kila wilaya, sisi tumekaa kwenye wilaya hizo. Hii migogoro tunajua kuna mifumo yaoke ya kumalizia huko, wakikosa staha wakatoka nje.”

Tarehe 19 Mei mwaka huu, Kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, kiliingia kwenye dosari baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya Meya wa manispaa hiyo, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wake, Sipora Liana.

Songoro Mnyonge, Meya wa Manispaa ya Kinondoni

Mvutano huo uliibuka baada ya Sipora, kutuhumu kwamba katika manispaa hiyo kuna genge la wezi, akidai kuna mtandao wa wizi wa fedha za ushuru wa takataka.

Kufuatia tuhuma hizo, Songoro alimtaka atoe ushahidi katika kikao hicho, juu ya tuhuma hizo ili vyombo vya ulinzi na usalama vichukue hatua.

Baada ya kauli hiyo, Sipora alisema ana uthibitisho kuhusu sakata hilo, akidai kuwa alifanya uchunguzi uliobainisha namna baadhi ya watendaji wa manispaa hiyo, wanavyofanya ubadhirifu katika ukusanyaji wa ushuru wa takatakata.

Mkurugenzi huyo wa Kinondoni alidai, watendaji hao wasiokuwa waaminifu huwapa risiti wananchi zenye viwnago vidiogo ikilinganishwa na fedha wanazotozwa.

“Wale watu walikuwa wamepewa kazi ya kukusanya mapato ya takataka, wakawa wanatoza wananchi 2,000, 1,000 na 3,000 lakini risiti wanazotoa zimeandikwa 100, 200 na 300. Wananchi wakaandamana kuja ofisini kwangu wakaleta risiti,” alisema Liana.

Liana alisema “nikatuma watu wangu kuchunguza wakabaini ni kweli wananachi wamelipa 1,000, 2,000 na 3,000. Tukaja kwenye mfumo wa kaprinti kuanzia mwaka jana Julai, tukaona katika kila risiti wamechukua 900, 1,800 na 2700.”

Kwa upande wa mvutano baina ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori na baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Ubungo, uliibuka baada ya madiwani hao kutuhumu Makori anajenga chuki baina yao.

Tuhuma hizo zilisababisha Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wilayani Ubungo, kilichofanyika tarehe 17 Mei mwaka huu, kuvunjika baada ya amdiwani hao kutaka kumpiga Makori.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

Regina Mkonde: CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!