Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo akemea upendeleo serikalini
Habari za Siasa

Chongolo akemea upendeleo serikalini

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Daniel Chongolo
Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali kupanga watumishi wa umma kwenye vituo vya kazi vya mjini kwa upendeleo wa kujuana na kuwapangia wengine vituo vya vijijini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu … (endelea).

Kauli hiyo ameitoa leo Ijumaa tarehe 3 Juni, 2022 wilayani Busega katika Kata ya Mkula Mkoa wa Simiyu akihitimisha ziara yake mkoani humo ya kukagua uhai wa chama kwenye mashina na utekelezaji wa ilani kwenye miradi ya maendeleo.

Akikagua ujenzi wa kituo cha afya cha Mkula, kilichokamilika ujenzi wake uliogharimu Sh.400 milioni na kinachotarajiwa kuanza kutoa huduma tarehe 20 Juni 2022, Katibu Mkuu amekemea tabia ya kupanga watumishi katika vituo vya kazi kwa upendeleo.

“Tuache upendeleo wa kupanga watumishi wa umma, baadhi ya watendaji mnapanga kwa kuwalundika eneo moja la mjini kwa kuangalia kujuana, wengine mnawapanga vijijini, ni vyema mkawapanga kwa kuangalia mahitaji ya eneo kwa sababu vituo vyote vya kazi vinahudumia wananchi na wote wanahitaji huduma,”amesema Chongolo.

1 Comment

  • Asante ndugu chongolo lakini uwelewo kuwa upendeleo upo ngazi zote ktk taifa letu wengine wamepewa vio vikubwa kwa upendeleo nawala hawatimizi wajibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!