June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chiragwile: Professa Muhongo ni mzigo usiobebeka

Spread the love

MGOMBEA ubunge Jimbo la Musoma Vijijini (Chadema), Mburaa Chiragwile amesema aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, ni mzigo usiobebeka kutokana na kulisababishia Taifa hasara ya Sh. 320 bil. Anaandika Moses Mseti, Musoma … (endelea).

Prof. Muhongo ambaye anagombea Jimbo la Musoma vijijini kupitia CCM ni miongoni mwa vigogo walijiuzuru kwa shinikizo la bunge na wengine kuondolewa katika nafasi zao na Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Kata ya Mwilingo, Nyakatende na Kulwaki, Chiragwile amesema Muhongo ni miongoni mwa viongozi waliolisababishia Taifa hasara na kuwataka wananchi kuacha kumchagua pamoja na wagombea wengine wa CCM.

Amesema kuwa Muhongo amekuwa akipita katika kata na vijiji akijinasibu kwamba yeye ndie amepeleka umeme katika jimbo hilo jambo ambalo ni la uongo kwani fedha zilizopeleka umeme ni za wananchi wenyewe.

“Msindanganyike na uongo wa Muhongo, eti yeye ndiye ameleta umeme ni sisi wenyewe tuliouleta hapa, kwani unapopanda gari unachangia, kwenye kila lita moja ya mafuta ya taa, dizeli na petroli unayonunua unachangia Shilingi mia moja.

“Muhongo ni ‘tapeli’ mwaka 2007 hakuwepo hapa nchini na serikalini hakuwepo, alikuwa ni mtafiti wa wazungu na kipindi umeme ulipoanza kusambazwa 2011 hakuwepo, sasa leo anakuja kuomba kura kwa sababu ya umeme na wakati hakuuleta,” amesema Chiragwile.

Hata hivyo Chiragwile aliwashauli wananchi wa jimbo hilo kwamba wanapaswa kumuogopa Prof. Muhongo kama ugonjwa wa ‘ukoma’ kwani anaweza kusababisha umaskini wao kuongezeka zaidi.

Chiragwile alivitaja vipaumbele vyake atakavyovishughulikia endapo atachaguliwa kuwa mbunge ni afya kwa kujenga zahanati kila kata na kujenga hospitali ya wilaya, elimu bora katika kila kaya ikiwa ni pamoja na kujenga sekondari za bweni, kujenga barabara kwa kiwango cha rami kutoka Musoma mjini hadi jimboni humo.

Pia alivitaja vipaumbele vingine kuwa ni kusimamia shughuli za wavuvi ili kukusanya mapato makubwa, kuimalisha kilimo ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wakulima fursa za kuuza mazao yao.

error: Content is protected !!