March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

China yathibitisha kumshikiria Rais wa Interpol

Rais wa Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol), Meng Hongwei

Spread the love

NCHI ya China imethibitisha kumzuia Rais wa Shirika la Polisi wa Kimataifa (Interpol), Meng Hongwei ikidai kuwa anafanyiwa uchunguzi na Tume ya Kupambana na Rushwa juu ya tuhuma ya ukiukaji wa sheria inayomkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wakati hayo yakijiri, taarifa zinaeleza kwamba Interpol imepokea barua ya kujiuzulu kwa Meng kutoka katika ofisi ya rais.

Meng ambaye mara ya mwisho kuonekana katika makao makuu ya Interpol mjini Lyon nchini Ufaransa akielekea China ilikuwa Septemba 25 2018, alitarajiwa kuachia madaraka katika shirika hilo mwaka 2020.

Rais huyo wa Interpol alichaguliwa kushika wadhifa huo mwezi Novemba mwaka 2016 ambaye alikuwa raia wa kwanza wa China kushikilia wadhifa huo.

error: Content is protected !!