Monday , 22 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya China, Tanzania kuboresha upasuaji ubongo MOI
Afya

China, Tanzania kuboresha upasuaji ubongo MOI

Hospitali ya Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI)
Spread the love

RAIS John Magufuli amefanya mazungumzo na Profesa Zhao Yuanil, Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Ubongo na Mishipa kutoka China kuhusu uboreshaji huduma ya  upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 26 Februari 2019  Ikulu jijini Dar es Salaam. Prof. Yuanil anatoka katika Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking (PUIH) iliyopo Beijing, China.

Mazungumzo hayo yamelenga kuboresha huduma hiyo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu ya Muhimbili (MOI).

Pia mazungumzo hayo yamehudhuria na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke, Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbil, Profesa Lawrence Mseru.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Magufuli amemuomba Prof. Yuanil kuwaleta watalaamu kutoka katika hospitali yake ili waje kutoa nhuduma na kuwafundisha madaktari wa Tanzania.

“Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na taarifa za kufanikiwa kwa mafanikio kwa upasuaji wa kwanza uliofanywa na Daktari Bingwa, Prof. Yuanil hapo jana, na kwamba anaamini wataalamu zaidi wataendelea kuja hapa nchini kutoka PUIH kwa ajili ya kutoa huduma za kuwafundisha madakrati wa Tanzania na pia watanzania wengi watakwenda nchini China kujifunza upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, amemhakikishia Prof. Yuanil kwamba serikali iko tayari kutoa ushirikiano utakaowezesha MOI kuongeza uwezo wake wa kutoa huduma za upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa Watanzania ambao wamekuwa wakikosa huduma hiyo ama kulazimika kutumia gharama kubwa kwenda nje ya nchi kufuata matibabu hayo.

Prof. Yuanil amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha MOI inaimarishwa ikiwemo kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu na amemhakikishia kuwa PUIH itahakikisha makubaliano yaliyotiwa saini mwaka jana kati ya hospitali hiyo na Wizara ya Afya, yanatekelezwa kikamilifu.

Naye, Ummy amemshukuru Rais Magufuli ka jitihada zake za kuwatafuta madaktari bingwa kutoka PUIH na kutoa maelekezo ya kuanzishwa kwa ushirikiano na MOI pamoja na kuhakikisha serikali inatoa zaidi ya shilingi bilioni 12.3 za kuimarisha miundombinu ya MOI ili itoe matibabu ya kibingwa ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa watanzania wengi.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk. Respicious Boniface amesmea kupitia ushirikiano huo Tanzania inatarajia kup[ata watalaamu wengi wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!