September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

China kuwasomesha wataalam wa gesi

Spread the love

SERIKALI ya China imetoa ufadhili kwa wanafunzi 20 kutoka nchini Tanzania kwa ajili ya kwenda China kusoma masuala yahusuyo mafuta na gesi. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dk. Hamisi Mwinyimvua ambapo amesema kuwa ufadhili huo ni kutokana na juhudi za serikali kuhakikisha wanapata ufadhili wa serikali ya China baada ya kugundua kuwa kuna upungufu wa wataalam wa mafuta na gesi nchini.

“Sasa hivi kuna gesi ambayo tumeshaanza kuitumia hapa nchini lakini pia kuna gesi imegundulika maeneo mbalimbali ya nchi hasa kwenye kina kirefu cha baharini, changamoto ambayo ilionekana baada ya kugundua gesi hii ni kwamba hatuba watalaam wa kutosha.

“Tulianza juhudi mbalimbali kupeleka wanafunzi nje kupitia fedha zinazochangiwa na mashirika mbalimbali yanayotafut mafuta na kuchimba gesi pia tumepata ufadhili kutoka China,” amesema.

Aidha amesema kuwa wanafunzi hao 20 watakaosoma digrii ya kwanza ni wawili, digrii ya pili ya udhamiri na 15 na digrii ya Uzamivu (PhD) ni wanafunzi watatu.

Kwa mujibu wa Dk. Mwinyimvua, Idadi hiyo inakamilisha kufikia idadi ya jumla ya wanafunzi 100 ambao wamefadhiliwa tangu kuanzishwa kwa programu hiyo ya ufadhili mwaka 2013.

error: Content is protected !!