September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

China kuisaidia Tanzania kudhibiti Corona

Spread the love

NCHI ya China imeahidi kuisadia Tanzania katika kudhibiti mlipuko wa Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo tarehe 25 Machi 2020, na Ubalozi wa China Nchini Tanzania, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Ubalozi huo umesema hayo wakati ikitoa taarifa ya ujio wa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kupambana na COVID-19, kutoka kwa taasisi ya bilionea wa nchi hiyo, Jack Ma.

Vifaa tiba hivyo ni vipimo 20,000, mavazi ya kujilinda 1,000 na barakoa (Mask) 100,000.

Ubalozi wa China umesema msaada huo ni muendelezo wa ukarimu wa taifa hilo, katika kusaidia nchi nyingine.

“Ndege ya Ethiopia iliyobeba barakoa 100,000, vipimo 20,000 na mavazi ya kujikinga 1,000, vilivyotolewa na Jack Ma, imewasili Dar es Salaam. Usambazaji huu unaashiria tamaduni ya utoaji wa China . China itatoa msaada zaidi katika mapigano ya Tanzania,” inaeleza taarifa ya Ubalozi huo.

error: Content is protected !!